> Kukarabati Kichapishi > Kuboresha Ubora wa Uchapishaji, Nakala na Utambazaji > Kusafisha Glasi ya Kitambazaji na Zulia ya Hali

Kusafisha Glasi ya Kitambazaji na Zulia ya Hali

Yafuatayo yanapofanyika, safisha glasi ya kitambazaji na zulia ya hati.

  • Nakala au taswira zilizotambazwa zikiwa zimepakwa mafuta

  • Wakati nakala au eneo lililotambazwa likienea ili kujumuisha uchafu au madoa, na kusababisha kunakili visivyo au nafasi isiyo sawa ya utambazaji au taswira ndogo

Tahadhari:

Chunga usijibane mkono au vidole wakati unafungua au kufunga kifuniko cha hati. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

Muhimu:

Usiwahi kutumia pombe au thina kusafisha printa. Kemikali hizi zinaweza kuharibu printa.

  1. Fungua kifuniko cha hati.

  2. Tumia kitambaa laini, safi na kikavu kusafisha eneo la glasi ya kitambazaji.

    Muhimu:
    • Iwapo eneo la kioo limekwamiliwa na grisi au nyenzo nyingine ngumu kuondoa, tumia kiasi kidogo cha kisafishaji kioo na kitambaa laini kuiondoa. Pangusa unyevu wote unaobakia.

    • Usibonyeze glasi kwa nguvu.

    • Kuwa makini usikwaruze au kuharibu glasi. Glasi iliyoharibika inaweza kupunguza ubora wa utambazaji.

  3. Safisha eneo la zulia la hati kwa kutumia nguo laini, safi na yenye unyevunyevu uliowekwa kwa kutumia sabuni kolezi.

  4. Pangusa zulia ya hati kwa kutumia nguo kavu.

    Tumia kitambazaji baada ya zulia ya hati kukauka.