> Kutatua Matatizo > Ni Wakati wa Kujaza tena Wino > Kujaza Tangi la Wino Upya

Kujaza Tangi la Wino Upya

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Jaza Wino.

  3. Soma tahadhari za matumizi za kujaza wino kwenye skrini, na kisha uende kwenye skrini inayofuata.

  4. Fungua kifuniko cha tanki la wino.

  5. Fungua kifuniko cha tanki la wino.

  6. Unaposhikilia chupa ya wino wima, geuza kifuniko polepole ili kukiondoa.

    Muhimu:
    • Epson inapendekeza utumie chupa halali za wino za Epson.

    • Chunga usimwage wino wowote.

  7. Angalia mstari wa juu (a) kwenye tanki la wino.

  8. Pangilia upande wa juu wa chupa ya wino kwa kituo cha kujaza, na kisha uichomeke wima kwenye kituo cha kujaza wino hadi usitishe kiotomatiki kwenye mstari wa juu.

    Wino utaanza kumwagika na mtiririko utakoma kiotomatiki wakati wino umefikia mstari wa juu.

    Iwapo wino hautaanza kutiririka kwenye tanki, ondoa chupa ya wino na ujaribu kuichomeka tena. Hata hivyo, usichomeke upya chupa ya wino wakati wino umefikia mstari wa juu zaidi; vinginevyo wino unaweza kuvuja.

  9. Baada ya kumaliza kujaza upya wino, ondoa chupa ya wino, na kisha ufunge kifuniko cha tanki la wino kwa usalama.

    Muhimu:

    Usiache chupa ya wino kama imechomekwa; vinginevyo huenda chupa ikaharibika au wino unaweza kumwagika.

    Kumbuka:

    Iwapo wino wowote utasalia kwenye chupa ya wino, kaza kifuniko na uhifadhi cvhupa ikisimama kwa matumizi ya baadaye.

  10. Funga kifuniko cha tanki la wino kabisa.

  11. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kuweka kiwango cha wino.

Muhimu:

Hata kama hutajaza wino hadi mstari wa juu wa tanki la wino, unaweza kuendelea kutumia kichapishi. Ili kufanya kichapishi chako kiendelee kufanya kazi kwa hali nzuri, hata hivyo, jaza upya tanki la wino hadi mstari wa juu na kisha uweke upya viwango vya wino mara moja.