Teua Mapendeleo ya Mfumo kutoka kwenye menyu ya Apple > Vichapishi na Vitambazaji (au Chapisho na Tambazo, Chapisho na Faksi).
Bofya +, na kisha uteue kichapishi chako kwenye skrini inayoonyeshwa.
Teua kichapishi chako kutoka Matumizi.
Bofya Ongeza.
Iwapo kichapishi hakijaorodheshwa, thibitisha kuwa kimeunganishwa sahihi kwenye kompyuta na kuwa kichapishi kimewashwa.