Kurekebisha Ubora wa Chapisho

Iwapo utagundua mistari wima isiyopangwa vizuri, taswira zisizoonekana vizuri, au mistari mlalo inayoonekana kwa umbali, rekebisha ubora wa chapisho.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Urekebishaji wa Ubora wa Chapa.

  3. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kupakia na kuchapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli.

  4. Chunguza muundo uliochapishwa.

    • Iwapo kuna mistari iliyotengana au sehemu zinazokosekana kama ilivyooshwa kwenye ruwaza ya “NG”, huenda nozeli za kichwa cha uchapishaji imeziba. Teua ili kusafisha kichwa cha kuchapisha.
    • Iwapo huwezi kuona mistari ya vitone au sehemu inayokosekana kama kwenye ruwaza inayofuata “OK”, nozeli haijaziba. Teua ili kuendelea kwa marekebisho yanayofuata.
  5. Fuata maagizo kwenye skrini ili kuchapisha ruwaza ya mpangilio wa kichwa cha chapisho, na kisha pangilia kichwa cha kuchapisha.

    • Ruwaza hii huekuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo machapisho yako hayaonekani vizuri.
      Tafuta na uteue nambari ya ruwaza imara zaidi.
    • Ruwaza hii hurukuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo mistari wima iliyopigiliwa itaonekana kutopangiliwa vizuri.
      Tafuta na uteue idadi ya ruwaza ambayo ina mstari michache wima isiyopangiliwa vizuri.
    • Ruwaza hii hukuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo utaona mistari mlalo inayoonekana kwa mbali katika vipindi vya muda wa kawaida.
      Tafuta na uteue nambari ya ruwaza iliyogawanywa na inayopishana.