Kuunda Akaunti ya Mtumiaji

Unda akaunti ya mtumiaji kwa udhibiti wa ufikiaji.

  1. Fikia Web Config na uteue kichupo cha Product Security > Access Control Settings > User Settings.

  2. Bofya Add kwa nambari unayotaka kusajili.

    Muhimu:

    Unapotumia kichapishi kwa mfumo wa uhalalishaji wa Epson au kampuni nyingine, sajili jina la mtumiaji la mpangilio wa uzuiaji kwenye nambari 2 hadi nambari 10.

    Programu-tumizi kama vile mfumo wa uhalalishaji hutumia nambari moja, ili jina la mtumiaji lisionyeshwe kwenye paneli ya udhibiti ya kichapishi.

  3. Weka kila kipengee.

    • User Name:
      Ingiza jina linaloonyeshwa kwenye orodfha ya jina la mtumiaji kati ya kibambo 1 na 14 kwa urefu kwa kutumia vibambo vya alfanumeriki.
    • Password:
      Ingiza nenosiri kati ya vibambo 0 na 20 kwa urefu kwenye ASCII (0x20–0x7E). Unapoanzisha nenosiri, liache wazi.
    • Select the check box to enable or disable each function.
      Teua kitendaji unachotaka kutumia.
  4. Bofya Apply.

    Rudi kwenye orodha ya mpangilio wa mtumijai baada ya kipindi maalum cha muda.

    Hakikisha kuwa jina la mtumiaji ulilolisajili kwenye User Name limeonyeshwa na kubadilishwa Add hadi Edit.