> Utambazaji > Kutambaza Nakala Asili kwenye Kifaa cha Kumbukumbu > Chaguo za Menyu Mahiri za Kutambaza kwenye Kifaa cha Kumbukumbu

Chaguo za Menyu Mahiri za Kutambaza kwenye Kifaa cha Kumbukumbu

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Mwelekeo (Asili):

Teua mwelekeo wa nakala asili.

Na. Asili zina Mch'o:

Unaweza kuweka mchanganyiko ufuatao wa ukubwa kwenye ADF kwa wakati mmoja. A3 na A4; B4 na B5. Unapotumia michanganyiko hii, nakala asili zinatambazwa kwa ukubwa halisi wa nakala asili. Weka nakala zako asili kwa kupanga upana wa nakala asili kama ilivyoonyeshwa hapa chini.

Uzito:

Teua ulinganuzi wa taswira iliyotambazwa.

Ondoa Kivuli:

Ondoa vivuli vya nakala asili ya ambavyo vinaonekana katika taswira iliyotambazwa.

  • Fremu:

    Ondoa vivuli katika ukingo wa nakala asili.

  • Katikati:

    Ondoa vivuli vya pambizo za kuweka pamoja vya kijitabu.

Ond. Mas'o ya Panchi:

Ondoa mashimo ya panji ambayo yanaonekana kwenye taswira iliyotambazwa. Unaweza kubainisha eneo la kufuta mashimo ya panji kwa kuingiza thamani kwenye kikasha upande wa kulia.

  • Mkao wa Kufuta:

    Teua mkao ili kuondoa mashimo.

  • Mwelekeo (Asili):

    Teua mwelekeo wa nakala asili.

Jina la Faili:
  • Kiambishi awali cha Jina la faili:

    Ingiza kiambishi awali cha jina la taswira katika vibambo vya alfanumeriki na alama.

  • Ongeza Tarehe:

    Ongeza tarehe ya jina la faili.

  • Ongeza Muda:

    Ongeza muda kwenye jina la faili.