Unaweza kuangalia takriban ya maisha ya huduma ya kikasha cha matengenezo kutoka kwenye paneli dhibiti. Bonyeza kitufe cha
, na kisha uchague Hali ya Printa.
Ili uhakikishe wino unaobakia, angalia viwango vya wino katika tangi la kichapishi.
Pia unaweza kuangalia makadirio ya viwango vya wino na makadirio ya maisha ya huduma ya kisanduku cha matengenezo kutoka kwenye kiwambo cha hali kwewnye kiendeshi cha kichapishi.
Windows
Bofya EPSON Status Monitor 3 kwenye kichupo cha Utunzaji.
Ikiwa EPSON Status Monitor 3 imelemazwa, bofya Mipangilio Iliyorefushwa kwenye kichupo cha Utunzaji, na kisha uteue Wezesha EPSON Status Monitor 3.
Mac OS
Apple menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi) > Epson(XXXX) > Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishaji > EPSON Status Monitor