> Kutatua Matatizo > Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Taa kwenye peneli ya udhibiti zinaonyesha hali ya kichapishi.

Hali ya Kawaida

: Washa

Taa

Hali

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi).

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa modi ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).

Hali ya Kosa

Wakati hitilafu zinatokea, taa huwaka au kumwekamweka. Maelezo ya hitilafu huonekana kwenye skrini ya kompyuta.

: Washa

: Inamwekamweka

Taa

Hali

Suluhisho

Hitilafu ya muunganisho wa Wi-Fi imetokea.

Bonyeza kitufe cha ili utatue hitilafu na ujaribu tena.

Hakuna karatsi imewekwa au zaidi ya karatasi moja zimeingizwa kwa wakati mmoja.

Weka karatasi na ubonyeze kitufe cha .

Karatasi imekwama.

Ondoa karatasi na ubonyeze kitufe cha .

Huenda ujazaji wa wino wa mwanzo haujakamilika.

Angalia bango la Anza Hapa ukamilishe ujazaji wa wino wa mwanzo.

Kikasha cha matengenezo kinakaribia mwisho wake wa kutoa huduma.

Mwangaza huendelea kumweka hadi kikasha cha matengenezo kibadilishwe.

Unaweza kuendelea kuchapisha hadi miangaza ya na inamweka moja baada ya mwingine.

  • Kichapishi hakikuzimwa vilivyo.*

  • Kwa kuwa kichapishi kilixzimwa kilipokuwa kikiendesha shughuli, huenda nozeli zimekauka na kuziba.

* Nishati ilizimwa kwa uknada au kitenganishaji cha nishati, plagi iliondolewa kwenye towe, au tatizo la umeme lilitokea.

  • Baada ya kuondoa kosa kwa kubonyeza kitufe cha , tunapendekeza utekeleze ukakuaji nozeli.

  • Ili kuzima kichapishi, hakikisha umebonyeza kitufe cha .

Kumweka kwa kubadilika:

Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Pedi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka inahitaji kubadilishwa.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili kubadlisha pedi ya wino ya uchapishaji usio na mpaka *. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Wakati ujumbe unaosema kwamba unaweza kuendelea kuchapisha unaonekana kwenye kompyuta, bonyeza ili uendelee kuchapisha. Taa zitawacha kumwekamweka kwa muda, hata hivyo, zitaendelea kumwekamweka mara kwa mara hadi padi ya wino ibadilishwe.

Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana.

Kumweka sawia:

Pedi ya wino iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Pedi ya wino inahitaji kubadilishwa. Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili ubadilishe pedi ya wino. Pedi za wino sio vyombo vinavyoweza kukarabatiwa na mtumiaji.

Angalia ujumbe ulioonyeshwa kwenye kompyuta, na kisha ubonyeze kitufe cha ili kuondoa hitilafu au ili kuendelea na usafishaji.

Iwapo pedi ya wino imefikia mwisho wake wa kutoa huduma, hauwezi tena kutekeleza usafishaji. Uchapishaji unaweza kutekelezwa lakini ubora wa machapisho hauwezi kuahidiwa.

Kufuli la usafirishaji imefungwa.

Baada ya kufungua kufuli la usafirishaji, bonyeza kitufe cha ili kuendelea kuchapisha.

Kumweka kwa kubadilika:

Mojawapo ya matatizo yafuatayo yametokea:

  • Usafishaji wa Nishati au Usafishaji wa Kichwa cha Kuchapisha haiwezi kutekelezwa kwa sababu hakuna nafasi tupu ya kutosha katika kikasha cha matengenezo.

  • Kikasha cha matengenezo hakijasakinishwa vizuri.

  • Kikasha cha matengenezo kimekaribia mwisho wa maisha yake ya kutoa huduma.

Fanya moja kati ya zifuatazo.

Unapoendesha Usafishaji wa Nishati au Usafishaji wa Kichwa cha Kuchapisha:

  • Badilisha kikasha cha matengenezo, bonyeza kitufe cha ili uondoe hitilafu, na kisha ujaribu tena.

  • Bonyeza kitufe cha ili kuondoa hitilafu ikiwa hauwezi kutayarisha kikasha cha matengenezo kinachobadilishwa mara moja. Uchapishaji unaweza kutekelezwa lakini ubora wa machapisho hauwezi kuahidiwa. Ikiwa tatizo litaendelea kutokea, badilisha kikasha cha matengenezo, na kisha ubonyeze kitufe cha .

Kando na yaliyo hapo juu:

Baada ya kusakinisha upya kikasha cha matengenezo vizuri, bonyeza kitufe cha . Ikiwa tatizo litaendelea kutokea baada ya kusakinisha upya, badilisha kikasha cha matengenezo, na kisha ubonyeze kitufe cha .

Miangaza yote itawaka isipokuwa mwangaza wa .

Kichapishi kimeanza katika modi ya kurejesha kwa sababu sasisho la programu msingi halijafaulu.

Fuata hatua zilizo hapa chini ujaribu kusasisha ngome tena.

1. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya USB. (Wakati wa modi ya kurejesha, huwezi kusasisha programu msingi kupitia muunganisho wa mtandao.)

2. Tembelea tovuti yako ya Epson kwa maelekezo zaidi.

Miangaza yote inawaka ikijumuisha mwangaza wa .

Hitilafu ya printa imetokea.

Ondoa karatasi yoyote ndani ya printa. Zima na uwashe printa tena.

Ikiwa hitilafu itaendelea kuonekana baada ya kuzima nishati na kuwasha tena, wasiliana na usaidizi wa Epson.

* Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mpaka. Pamoja na kutumia kikasha cha matengenezo, pedi hii ya wino hufyonza wino usiotumiwa unaotolewa wakati unatumia kichapishi. Wakati pedi imefikia mwisho wa maisha yake ya kutoa huduma, kusafisha hakuwezi kutekelezwa hadi pedi ibadilishwe. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha ukitumia chaguo la kuchapisha bila kingo. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.