> Kukarabati Kichapishi > Kuboresha Ubora wa Uchapishaji > Kusafisha Njia ya Karatasi kwa Kupaka Wino (wakati Eneo la Nyuma la Matokeo ya Uchapishaji Limepakwa Wima)

Kusafisha Njia ya Karatasi kwa Kupaka Wino (wakati Eneo la Nyuma la Matokeo ya Uchapishaji Limepakwa Wima)

Wakati uchapishaji una uchafu au kuchakaa, safisha kibiringizaji kiicho ndani.

Unahitaji ufagio wa pamba ili kutekeleza taratibu kutoka kwa hatua ya 2.

  1. Tekeleza Usafishaji wa Mwongozo wa Karatasi kutoka kwa kiendeshi cha kichapishi ili kusafisha njia ya karatasi.

    • Windows
      Fikia dirisha la kiendeshi cha kichapishi, kisha bofya Usafishaji wa Mwongozo wa Kratasi kwenye kichupo cha Utunzaji. Fuata maagizo ya kwenye skrini.
    • Mac OS
      Teua Mapendeleo ya Mfumo kwenye menyu ya Apple > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi), na kisha uteue kichapishi. Bofya Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishi, na kisha bofya Paper Guide Cleaning. Fuata maagizo ya kwenye skrini.

    Rudia utaratibu ulio hapo juu hadi karatasi iwache kuchafuliwa na wino.

  2. Wakati tatizo haliwezi kuondolewa baada ya kusafisha njia ya karatasi, sehemu iliyo ndani ya kichapishi ambayo imeonyeshwa kwenye kielelezo inalainishwa. Zima kichapishi, na kisha upanguse wino kwa kutumia pamba.

    Muhimu:
    • Usitumie karatasi ya shashi kusafisha ndani ya kichapishi. Nozeli za kichwa cha kushapisha zinaweza kuzibwa na nyuzi za pamba.

    • Usiguze kebo nyeupe bapa, sehemu angavu, na tyubu za wino zilizo ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.