> Kutatua Matatizo > Karatasi Zinakwama > Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Tahadhari:

Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi. Ikiwa kichapishi kitaanza kufanya kazi, inaweza kusababisha majeraha. Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.

  1. Ondoa karatasi iliyokwama.

  2. Fungua kifuniko cha mbele.

  3. Fungua kifuniko cha kichapishi hadi kitoe mbofyo.

    Muhimu:

    Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye mfano ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  4. Ondoa karatasi iliyokwama.

    Muhimu:

    Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye mfano ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  5. Funga kifuniko cha kichapishi.

    Kwa usalama, kifuniko cha kichapishi kinafungwa kwa hatua mbili.

    Kumbuka:

    Lazima kifuniko cha kichapishi kiwe kimefungwa kabisa kabla ya kufunguka tena.

  6. Funga kifuniko cha mbele.