> Kuweka Karatasi > Kupakia Karatasi > Kupakia Karatasi katika Trei ya Karatasi

Kupakia Karatasi katika Trei ya Karatasi

  1. Vuta nje auni ya karatasi.

  2. Telezesha miongozo ya kingo.

  3. Pakia karatasi katikati ya auni ya karatasi huku upande unaweza kuchapishwa ukiangalia juu.

  4. Telezesha miongozo ya kingo kwenye ukingo wa karatasi.

  5. Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi.

    Mipangilio ya Ukubwa na Aina ya Karatasi

    Kumbuka:
    • Kwa karatasi ya kichwa cha barua, teua Letterhead kama aina ya karatasi.

    • Kwa karatasi ya kichwa cha barua, iwapo utachapisha kwenye karatasi ambayo ni ndogo kuliko mpangilio kwenye kiendeshi cha kichapishi, huenda kichapishi kikachapisha zaidi ya kingo za karatasi zinazoweza kusababisha uchafu wa wino kwenye machapisho yako na wino zaidi kuongezeka ndani ya kichapishi. Hakikisha kuwa unateua mpangilio wa ukubwa sahihi wa karatasi.

    • Uchapishaji wa pande 2 na uchapishaji usio na kingo haupatikani kwa karatasi yenye mwambaa kichwa. Pia, huenda kasi ya uchapishaji ikapungua.

  6. Toa trei ya kushikilia nakala zinazochapishwa.

    Kumbuka:

    Rudisha karatasi zinazosalia kwenye paketi. Ukiziwacha katika printa, karatasi hizo zinaweza kukunjika au ubora wa uchapishaji unaweza kupungua.