Kukatisha Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi)

Kuna mbinu mbili zinazopatikana za kulemaza muuganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi); unaweza kulemaza miunganisho yote kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, au kulemaza kila muunganisho kutoka kwenye kompyuta au kifaa maizi. Sehemu hii hufafanua jinsi ya kulemaza miunganisho yote.

Muhimu:

Wakati muunganisho wa Wi-Fi Direct wa (AP Rahisi) unalemazwa, kompyuta zote na vifaa maizi vilivyounganishwa kwenye kichapishi katika muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) vinatenganishwa.

Kumbuka:

Iwapo unataka kukata muunganisho wa kifaa maalum, kata muunganisho kutoka kwenye kifaa badala ya kichapishi. Tumia mojawapo ya mbinu zifuatazo ili kukata muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) kutoka kwenye kifaa.

  • Kata muunganisho wa Wi-Fi kwenye jina la mtandao la kichapishi (SSID).

  • Unganisha kwenye jina jingine la mtandao (SSID).

  1. Donoa kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Teua Wi-Fi Direct.

    Maelezo ya Wi-Fi Direct yanaonyeshwa.

  3. Donoa Anza Kusanidi.

  4. Donoa Badilisha.

  5. Teua Lemaza Wi-Fi Direct.

  6. Donoa Lemaza mipangilio.

  7. Wakati ujumbe wa ukamilisho umeonyeshwa, funga skrini.

    Skrini hufunga kiotomatiki baada ya kipindi maalum cha muda.

  8. Funga skrini ya Mipangilio ya Muunganis. Mtandao.