> Kunakili > Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili

Chaguo Mahiri za Menyu kwa Kunakili

Kumbuka:

Huenda vipengee visipatikane kulingana na mipangilio mingine uliyofanya.

Mipangilio ya K'si:

Chagua chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia. Wakati Otomatiki imeteuliwa, karatasi linaingizwa kiotomatiki kwa kutumia mipangilio ya Mipangilio ya Karatasi iliyoundwa ulipopakia karatasi.

Kuza:

Husanidi mgao wa ukuzaji wa upanuaji au upunguzaji. Donoa thamani na ubainishe ukuzaji unaotumika kuongeza au kupunguza nakala asili ndani ya masafa ya 25 hadi 400%.

  • Saizi Halisi

    Hunakili kwa ukuzaji wa 100%.

  • A4→A5 na nyingine

    Hukuza au kupunguza nakala asili kiotomatiki ili kutoshea kwenye ukubwa wa karatasi bainifu.

  • Tosheza Ukrs Oto

    Hutambua eneo la kuchapisha na kukuza kiotomatiki au kupunguza nakala asili ili itoshee kwenye ukubwa wa karatasi uliyoteua. Wakati kuna pambizo nyeupe kwenye nakala asili, pambizo hizo nyeupe kutoka kwenye alama ya kona ya kioo cha kitambazaji zinatambuliwa kama eneo la kutambaza, lakini pambizo katika upande mkabala zinaweza kupunwa.

Saizi ya Hati:

Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza. Unaponakili nakala asili za ukubwa usio wastani, teua ukubwa unaokaribiana na nakala yako asili.

Kurasa Nyingi:

Teua muundo wa nakala.

  • Ukurasa Mmoja

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.

  • 2-juu

    Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.

Ubora:

Teua ubora wa nakili. Kuteua Juu hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa ya chini.

Mwelekeo wa Hati:

Teua mwelekeo wa nakala yako asili.

Ondoa Kivuli:

Huondoa vivuli vinavyoonekana kwenye nakala unaponakili karatasi nzito au vinavyotokea katikati ya nakala unaponakili kijitabu.

Ondoa Mashimo ya Panchi:

Huondoa mashino ya kufunga wakati wa kunakili.

Nakala ya Kadi ya ID:

Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi.

Nakala Isiyo na mipaka:

Hunakili bila pambizo kwenye kingo. Taswira imekuzwa kidogo ili kuondoa pambizo kutoka kwenye kingo za karatasi. Teua kiwango cha kubadilisha ukubwa kwenye mpangilio wa Upanuzi.

Ondoa Mipangilio Yote:

Rejesha mipangilio ya nakala kuwa chaguomsingi.