Haiwezi Kutuma au Kupokea Faksi Hata Ingawa Muunganisho Umewekwa Ipasavyo (Windows)

prPProgramu haijasakinishwa.

Suluhisho

Hakikisha kwamba kiendeshi cha PC-FAX kimesakinishwa kwenye kompyuta. Kiendeshi cha PC-FAX kimesakinishwa pamoja na FAX Utility. Fuata hatua za hapa chini ili kuangalia jiwapo kimesakinishwa.

Hakikisha kichapishi (faksi) kinaonekana katika Vifaa na Vichapishi, Kichapishi, au Kichapishi na Maunzi Mengine. Printa (faksi) inaonekana kama “EPSON XXXXX (FAX)”. Ikiwa kichapishi (faksi) hakionekani, sakinusha FAX Utility na kisha uisakinishe upya. Angalia yafuatayo ili ufikie Vifaa na Vichapishi, Kichapishi, au Vichapishi na Maunzi Mengine.

  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha kisha uchague Mifumo ya Windows > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Teua Eneo-kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti au Maunzi.

  • Windows 7

    Bofya kitufe cha kuanza, na uchague Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti au Maunzi.

  • Windows Vista

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Kichapishi katika Maunzi na Sauti.

  • Windows XP

    Bofya kitufe cha kuanza, na uchague Mipangilio > Paneli Dhibiti > Printa na Maunzi Mengine > Printa na Faksi.

UhalaliUhalalishaji wa mtumiaji umeshindikana wakati faksi imetumwa kutoka kwenye kompyuta.

Suluhisho

Weka jina la mtumiaji na nywila kwenye kiendeshi cha kichapishi. Unapotuma faksi kutoka kwenye kompyuta wakati kitendaji cha usalama kinachowauhusu wasimamizi kuwazuia watumiaji dhidi ya kubadilisha kitendaji cha faksi ya kichapishi kuwekwa, uhalalishaji wa mtumiaji unatekelezwa kwa jina la mtumiaji na nywila kama imewekwa kwenye kiendeshi cha kichapishi.

Kuna baadhi ya matatizo kwa muunganisho wa faksi na mipangilio ya faksi.

Suluhisho

Jaribu suluhisho za muunganisho wa faksi na mipangilio ya faksi.