Kurekebisha Ubora wa Chapisho

Iwapo utagundua mistari wima isiyopangwa vizuri, taswira zisizoonekana vizuri, au mistari mlalo inayoonekana kwa umbali, rekebisha ubora wa chapisho. Iwapo unataka kurekebisha ubora wa chapisho kwa karatasi, kwanza unda mpangilio huu. Thamani ya mpangilio kwa karatasi inawekwa upya iwapo utaunda mpangilio huu baada ya kurekebisha kwa karatasi.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Urekebishaji wa Ubora wa Chapa.

  3. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuangalia kichapishi ili kuboresha ubora wa chapisho.

    Iwapo ujumbe unaonyeshwa unaopendekeza kuwa usafishe kichwa cha kuchapisha, tekeleza usafishaji wa kichwa cha chapisho.

  4. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kupakia karatasi na kuchapisha ruwaza ya kupangilia kichwa cha kuchapisha

  5. Chunguza ruwaza zilizochapishewa na upangilie kichwa cha kuchapisha.

    • Ruwaza hii huekuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo machapisho yako hayaonekani vizuri.
      Tafuta na uteue nambari ya ruwaza imara zaidi.
    • Ruwaza hii hurukuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo mistari wima iliyopigiliwa itaonekana kutopangiliwa vizuri.
      Tafuta na uteue idadi ya ruwaza ambayo ina mstari michache wima isiyopangiliwa vizuri.
    • Ruwaza hii hukuruhusu kutekeleza mpangilio iwapo utaona mistari mlalo inayoonekana kwa mbali katika vipindi vya muda wa kawaida.
      Tafuta na uingize nambari ya ruwaza iliyogawanywa na inayopindana.