Kukagua na Kusafisha Kichwa cha Kuchapisha

Ikiwa nozeli zimeziba, uchapishaji unakuwa fifu, mistati inaonekana, au rangi zisizotarajiwa zinaonekana. Ikiwa nozeli zimeziba sana, karatasi tupu itachapishwa. Wakati ubora wa chapisho umepungua, kwanza tumia kipengele cha kukagua nozeli na ukague kama nozeli zimeziba. Ikiwa nozeli zimeziba, safisha kichwa cha kuchapisha.

Muhimu:
  • Usifungue kitengo cha kitambazo au kuzima printa wakati wa usafishaji wa kichwa. Ikiwa usafisha wa kichwa haujakamilika, huenda usiweze kuchapisha.

  • Kusafisha kichwa hutumia wino mwingi na unapaswa kufanywa ikiwa ni muhimu tu.

  • Wakati wino ni kidogo, huenda usiweze kusafisha kichwa cha kuchapisha.

  • Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kuangalia nozeli na kusafisha kichwa mara 3, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha kisha uangalie nozeli tena na urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni muhimu. Tunapendekeza uzime kichapishi kwa kutumia kitufe cha . Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati.

  • Ili kuzuia kichwa cha kuchapisha kisikaue, usichomoe printa wakati nishati imewashwa.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

  2. Teua Ukgz Nozeli ya Kichwa Chapa.

  3. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kupakia karatasi na kuchapisha ruwaza ya kukagua nozeli.

  4. Angalia ruwaza iliyochapishwa ili kuona iwapo nozeli za kichwa cha kuchapisha zimezibika.

    • A:
      Mistari yote imechapishwa. Teua . Hakuna hatua za ziada zinazohitajika.
    • B au karibu na B
      Baaadhi ya nozeli zimeziba. Teua , na kisha ufuate maagizo kwenye skrini ili kusafisha kichwa cha chapisho.
    • C au karibu na C
      Iiwa laini nyingi hazipo au hazijachapishwa, hii inaonyesha kwamba nozeli nyingi zimeziba. Teua ili kutoka kwenye kipengele cha kukagua nozeli, na kisha uendeshe Usafishaji wa Nishati. Kwa maelezo, tazama “Maelezo husiani” hapa chini.
  5. Usafishaji unapokamilika, chapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli tena. Rudia usafishaji na uchapishaji hadi mistari yote ichapishwe kabisa.

Muhimu:

Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kuangalia nozeli na kusafisha kichwa mara 3, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha kisha uangalie nozeli tena na urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni muhimu. Tunapendekeza uzime kichapishi kwa kutumia kitufe cha . Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati.

Kumbuka:

Unaweza kuangalia na kusafisha kichwa cha kuchapisha kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi.

  • Windows

    Bofya Ukaguzi wa Nozeli ya Kichwa cha Kuchapisha kwenye kichupo cha Utunzaji.

  • Mac OS

    Apple menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi) > Epson(XXXX) > Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishaji > Ukaguzi wa Nozeli ya Kichwa cha Kuchapisha