Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Mipangilio ya Jumla > Mipangilio Msingi
Huwezi kubadilisha mipangilio iliyozuiwa na msimamizi wako.
Mipangilio Msingi
Mwangaza wa LCD
Rekebisha mwangaza wa skrini ya LCD.
Sauti
Rekebisha sauti.
Nyamazisha
Teua On ili kunyamazisha sauti.
Hali ya Kawaida
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe.
Hali Tulivu
Teua sauti kama vile Ubonyezaji Kitufe kwenye Hali Tulivu.
Kipima saa cha Kulala
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Amsha
Gusa Skrini ya LCD Kuamsha
Chagua Washa urudi kwenye modi ya kulala (modi ya kuhifadhi nishati) kwa kugusa paneli ya mguso. Wakati imezimwa unahitaji kubonyeza kitufe kilicho kwenye paneli dhibiti ili uamshe printa. Kuzima kipengele hiki huzuia utendaji wowote usiokusudiwa kutokea kwa sababu ya vitu vya kigeni vinavyogusa skrini. Pia unaweza kuweka kipindi cha muda ambao kupengee hiki kimewasha.
Kipima Saa ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Mip'ilio ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha LINE kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Teua mpangilio wa wakati wa majira ya joto unaotumika katika eneo lako.
Utofauti wa Saa
Ingiza tofauti ya saa kati ya saa yako ya ndani na UTC (Saa Inayoratibiwa ya Kimataifa).
Nchi/Eneo
Teua nchi au eneo ambalo unatumia kichapishi chako. Iwapo utabadilisha nchi au eneo, mipangilio yako ya faksi inarejea kwa chaguo-msingi na lazima uiteue tena.
Lugha/Language
Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.
Skrini ya Kuanza
Bainisha menyu ya kwanza inayoonyeshwa kwenye skrini ya LCD wakati kichapishi kinawaka na Muda wa Shughuli Umeisha imewezeshwa.
Hariri Ukurasa wa Nyumbani
Badillisha muundo wa ikoni kwenye skrini ya LCD. Pia unaweza kuongeza, kuonmdoa, na kuhamisha ikoni.
Pazia
Badilisha rangi ya mandharinyuma ya skrini ya nyumbani.
Muda wa Shughuli Umeisha
Teua On ili kurejesha skrini ya kwanza wakati hakuna operesheni imetekelezwa kwa muda uliobainishwa. Wakati vizuizi vya mtumiaji vimewekwa na hakuna operesheni zinatekelezwa kwa muda uliobainishwa, unaondolewa na kurejeshwa kwenye skrini ya kwanza.
Kibodi
Badillisha muundo wa kibodi kwenye skrini ya LCD.
Skrini chaguo-msingi(Kazi/Hali)
Teua maelezo chaguo-msingi unayotaka kuonyesha unapobonyeza kitufe cha .
Chaguo la Utambuaji Oto wa Ukubwa Asili
ADF na glasi ya kitambazaji zina sensa ambazo hutambua otomatiki ukubwa wa karatasi. Hata hivyo, kutokana na mifano ya sensa, ukubwa sawa hauwezi kutambuliwa, na karatasi ya ukubwa wa K, ambayo inatumika zaidi China, haiwezi kutambuliwa sahihi katika hali ya awali ya kichapishi. Teua Kipaumbele cha Ukubwa wa K iwapo kila mara huwa unatumia ukubwa wa karatasi wa K. Ukubwa asili utatambuliwa kama ukubwa wa K badala ya ukubwa unaokaribia. Kutegemea ukubwa na mwelekeo wa karatasi, inaweza kugunduliwa kama ukubwa mwingine unaokaribia. Pia, ukubwa wa K unaweza kukosa kugunduliwa kutegemea kazi unayotumia. Kwa mfano, unapotambaza na kuhifadhi kwenye kompyuta kwa kutumia programu hiyo, kama au la ukubwa wa K unaweza kutambuliwa otomatiki kunategemea tabia ya programu hiyo.