> Mwongozo wa Paneli Dhibiti > Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Taa kwenye peneli ya udhibiti zinaonyesha hali ya kichapishi.

Hali ya Kawaida

: Washa

Taa

Hali

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi).

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa modi ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).

Hali ya Kosa

Wakati hitilafu zinatokea, taa huwaka au kumwekamweka. Maelezo ya hitilafu huonekana kwenye skrini ya kompyuta.

/: Washa

/: Inamwekamweka

Taa

Hali

Suluhisho

Hitilafu ya muunganisho wa Wi-Fi imetokea.

Bonyeza kitufe cha ili utatue hitilafu na ujaribu tena.

Huenda ujazaji wa wino wa mwanzo haujakamilika.

Angalia bango la Anza Hapa ukamilishe ujazaji wa wino wa mwanzo.

Hakuna karatsi imewekwa au zaidi ya karatasi moja zimeingizwa kwa wakati mmoja.

Weka karatasi na ubonyeze kitufe cha au .

Karatasi imekwama.

Ondoa karatasi na ubonyeze kitufe cha au .

Iwapo kosa la kukwama kwa karatasi litaendelea baada ya kuondoa karatasi na kuzima na kuwasha tena, huenda karatasi likasalia ndani ya kichapishi. Pakia karatasi ya ukubwa wa A4 kwenye mlisho wa nyuma wa karatasi, na kisha ubonyeze kitufe cha au ili kuondoa karatasi ndani. Pakia karatasi kwenye mwelekeo wa kurasa wima.

Iwapo kosa haliwezi kufutwa, wasiliana na auni ya Epson.

  • Kichapishi hakikuzimwa vilivyo.*

  • Kwa kuwa kichapishi kilixzimwa kilipokuwa kikiendesha shughuli, huenda nozeli zimekauka na kuziba.

* Nishati ilizimwa kwa uknada au kitenganishaji cha nishati, plagi iliondolewa kwenye towe, au tatizo la umeme lilitokea.

  • Baada ya kuondoa kosa kwa kubonyeza kitufe cha au , tunapendekeza utekeleze ukakuaji nozeli. Katisha kazi zozote za uchapishaji zilizopo.

  • Ili kuzima kichapishi, hakikisha umebonyeza kitufe cha .

Wakati taa ya na itamwekamweka kwa kubadilishana.

Pedi ya wino iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Padi za wino zinahitaji kubadilishwa.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson ili ubadilishe padi ya wino.*1 Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Wakati ujumbe unaosema kwamba unaweza kuendelea kuchapisha unaonekana kwenye kompyuta, bonyeza kitufe cha au ili uendelee kuchapisha. Taa zitawacha kumwekamweka kwa muda, hata hivyo, zitaendelea kumwekamweka mara kwa mara hadi padi ya wino ibadilishwe.

Wakati mwangaza wa na mwangaza wa hupepesa wakati tofauti

Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka inahitaji kubadilishwa.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson ili ubadilishe padi ya wino.*2 Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Wakati ujumbe unaosema kwamba unaweza kuendelea kuchapisha unaonekana kwenye kompyuta, bonyeza kitufe cha au ili uendelee kuchapisha. Taa zitawacha kumwekamweka kwa muda, hata hivyo, zitaendelea kumwekamweka mara kwa mara hadi padi ya wino ibadilishwe.

Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana.

Kichapishi kimeanza katika modi ya kurejesha kwa sababu sasisho la programu msingi halijafaulu.

Fuata hatua zilizo hapa chini ujaribu kusasisha ngome tena.

1. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya USB. (Wakati wa modi ya kurejesha, huwezi kusasisha programu msingi kupitia muunganisho wa mtandao.)

2. Tembelea tovuti yako ya Epson kwa maelekezo zaidi.

Hitilafu ya printa imetokea.

Ondoa karatasi yoyote ndani ya printa. Zima na uwashe printa tena.

Ikiwa hitilafu itaendelea kuonekana baada ya kuzima nishati na kuwasha tena, wasiliana na usaidizi wa Epson.

*1 Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino. Ili kuzuia uvujaji wa wino kutoka kwa padi, printa hii imeundwa kusimamisha uchapishaji wakati padi imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha, aina ya nyenzo unayochapisha na idadi ya mizunguko ya usafisha ambayo printa inafanya. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.

*2 Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mpaka. Ili kuzuia uvujaji wa wino kutoka kwenye padi, bidhaa hii imeundwa kusimamisha uchapishaji usiokuwa na mpaka wakati padi imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha ukitumia chaguo la kuchapisha bila kingo. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.