> Kuchapisha > Kuchapisha Nyaraka > Kuchapisha Nyaraka kutoka Vifaa Maizi (Android) > Kuchapisha Nyaraka kwa kutumia Epson Print Enabler

Kuchapisha Nyaraka kwa kutumia Epson Print Enabler

Kumbuka:

Uendeshaji unaweza kutofautiana kulingana na kifaa.

  1. Kwenye kifaa chako cha Android, sakinisha kiendelezi cha Epson Print Enabler kutoka Google Play.

  2. Nenda katika Mipangilio kwenye kifaa cha Android, teua Kuchapisha kisha wezesha Epson Print Enabler.

  3. Kutoka katika programu ya Android kama vile Chrome, donoa aikoni ya menyu na uchapishe kilicho kwenye skrini.

    Kumbuka:

    Iwapo hutaona kichapishi chako, donoa Vichapishi Vyote na uteue kichapishi chako.