> Kutatua Matatizo > Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Taa kwenye peneli ya udhibiti zinaonyesha hali ya kichapishi.

Hali ya Kawaida

: Washa

Taa

Hali

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi).

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa modi ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).

Kichapishi kimewekwa ili kuchapisha kwenye karatasi inayoashiriwa na mwangaza. Mpangilio huu unatumiwa tu wakati unachapisha kwa kutumia AirPrint au Mopria, ili uweze kupuuza mwangaza unapochapisha kwa kutumia mbinu zingine. Kwa maelezo zaidi, tazama ufafanuzi wa kitufe cha .

Hali ya Kosa

Wakati hitilafu zinatokea, taa huwaka au kumwekamweka. Maelezo ya hitilafu huonekana kwenye skrini ya kompyuta.

/: Washa

/: Inamwekamweka

Taa

Hali

Suluhisho

Hitilafu ya muunganisho wa Wi-Fi imetokea.

Bonyeza kitufe cha ili utatue hitilafu na ujaribu tena.

Huenda ujazaji wa wino wa mwanzo haujakamilika.

Angalia bango la Anza Hapa ukamilishe ujazaji wa wino wa mwanzo.

Hakuna karatsi imewekwa au zaidi ya karatasi moja zimeingizwa kwa wakati mmoja.

Weka karatasi na ubonyeze kitufe cha au .

Karatasi imekwama.

Ondoa karatasi na ubonyeze kitufe cha au .

Iwapo kosa la kukwama kwa karatasi litaendelea baada ya kuondoa karatasi na kuzima na kuwasha tena, huenda karatasi likasalia ndani ya kichapishi. Pakia karatasi ya ukubwa wa A4 kwenye mlisho wa nyuma wa karatasi, na kisha ubonyeze kitufe cha au ili kuondoa karatasi ndani. Pakia karatasi kwenye mwelekeo wa kurasa wima.

Iwapo kosa haliwezi kufutwa, wasiliana na auni ya Epson.

Kikasha cha matengenezo kinakaribia mwisho wake wa kutoa huduma.

Mwangaza huendelea kumweka hadi kikasha cha matengenezo kibadilishwe.

Unaweza kuendelea kuchapisha hadi miangaza ya na inamweka moja baada ya mwingine.

  • Kichapishi hakikuzimwa vilivyo.*

  • Kwa kuwa kichapishi kilixzimwa kilipokuwa kikiendesha shughuli, huenda nozeli zimekauka na kuziba.

* Nishati ilizimwa kwa uknada au kitenganishaji cha nishati, plagi iliondolewa kwenye towe, au tatizo la umeme lilitokea.

  • Baada ya kuondoa hitilafu kwa kubonyeza kitufe cha au , bonyeza kitufe cha ili kughairi kazi za uchapishaji zinazosubiriwa. Tunapendekeza utekeleze ukaguzi wa nozeli.

  • Ili kuzima kichapishi, hakikisha umebonyeza kitufe cha .

Kumweka kwa kubadilika:

Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Pedi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka inahitaji kubadilishwa.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili kubadlisha pedi ya wino ya uchapishaji usio na mpaka *. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Wakati ujumbe unaosema kwamba unaweza kuendelea kuchapisha unaonekana kwenye kompyuta, bonyeza kitufe cha au ili uendelee kuchapisha. Taa zitawacha kumwekamweka kwa muda, hata hivyo, zitaendelea kumwekamweka mara kwa mara hadi padi ya wino ibadilishwe.

Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana.

Kumweka sawia:

Pedi ya wino iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Pedi ya wino inahitaji kubadilishwa. Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili ubadilishe pedi ya wino. Pedi za wino sio vyombo vinavyoweza kukarabatiwa na mtumiaji.

Kagua ujumbe ulioonyeshwa kwenye kompyuta, na kisha bonyeza kitufe cha au ili kuondoa hitilafu au ili kuendelea na usafishaji.

Iwapo pedi ya wino imefikia mwisho wake wa kutoa huduma, hauwezi tena kutekeleza usafishaji. Uchapishaji unaweza kutekelezwa lakini ubora wa machapisho hauwezi kuahidiwa.

Kumweka kwa kubadilika:

Mojawapo ya masuala yafuatayo limefanyika tayari:

  • Usafishaji wa Nishati au kusafisha kichwa cha kichapishi hakuwezi kufanyika kwa sababu hakuna nafasi ya kutosha katika kisanduku cha usimamizi.

  • Kisanduku cha usimamizi hakijasakinishwa sahihi.

  • Kisanduku cha usimamizi kipo mwishoni mwa kipindi chake cha kuhudumu.

Fanya mojawapo ya yafuatayo.

Unapoendesha Usafishaji wa Nishati au kusafisha kichwa cha kichapishi:

  • Badilisha kisanduku cha usimamizi, bonyeza kitufe cha au ili kuondoa hitilafu hiyo, na kisha ujaribu tena.

  • Bonyeza kitufe cha au ili kuondoa hitilafu hiyo iwapo huwezi kuandaa kisanduku cha usimamizi cha kubadilisha mara moja. Hitilafu ikiendelea kufanyika, badilisha kisanduku cha usimamizi, na kisha ubonyeze kitufe cha au .

Kando na iliyo hapo juu:

Baada ya kusakinisha tena kisanduku cha usimamizi sahihi, bonyeza kitufe cha au .

Hitilafu ikiendelea kufanyika baada ya kusakinisha upya, badilisha kisanduku cha usimamizi, na kisha ubonyeze kitufe cha au .

Kifuniko cha trei ya towe hakijafunguliwa.

Fungua kifuniko cha trei ya towe, kisha utelezeshe trei ya towe nje.

Miangaza yote itawaka isipokuwa mwangaza wa .

Kichapishi kimeanza katika modi ya kurejesha kwa sababu sasisho la programu msingi halijafaulu.

Fuata hatua zilizo hapa chini ujaribu kusasisha ngome tena.

1. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya USB. (Wakati wa modi ya kurejesha, huwezi kusasisha programu msingi kupitia muunganisho wa mtandao.)

2. Tembelea tovuti yako ya Epson kwa maelekezo zaidi.

Miangaza yote inawaka ikijumuisha mwangaza wa .

Hitilafu ya printa imetokea.

Ondoa karatasi yoyote ndani ya printa. Zima na uwashe printa tena.

Ikiwa hitilafu itaendelea kuonekana baada ya kuzima nishati na kuwasha tena, wasiliana na usaidizi wa Epson.

* Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mpaka. Ili kuzuia uvujaji wa wino kutoka kwenye padi, bidhaa hii imeundwa kusimamisha uchapishaji usiokuwa na mpaka wakati padi imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha ukitumia chaguo la kuchapisha bila kingo. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.