> Kuweka Karatasi > Pakia Karatasi katika Mlisho wa Nyuma wa Karatasi

Pakia Karatasi katika Mlisho wa Nyuma wa Karatasi

  1. Vuta nje auni ya karatasi.

    ET-4800 Series/L5290 Series

    ET-2820 Series/L3260 Series

  2. Telezesha miongozo ya kingo.

  3. Pakia karatasi katikati ya auni ya karatasi huku upande unaweza kuchapishwa ukiangalia juu.

    Muhimu:
    • Usiweke zaidi ya upeo wa idadi ya karatasi uliotajwa kwa karatasi. Kwa karatasi tupu, usiweke karatasi hadi juu ya mstari uliochini ya alama ya upande wa dnani wa mwongozo wa kingo.

    • Pakia ukingo mfupi wa karatasi kwanza. Hata hivyo, wakati umeweka ukingo mrefu kama upana wa ukubwa wa mtumiaji uliofafanuliwa, pakia ukingo mrefu wa karatasi kwanza.

  4. Telezesha miongozo ya kingo kwenye ukingo wa karatasi.

    ET-2820 Series/L3260 Series: Funga kilinzi cha mlisho baada ya kutelezesha miongozo ya kingo.

    Muhimu:

    ET-2820 Series/L3260 Series: Usiweke vifaa kwenye kilinzi cha mlisho. Kufanya hivyo kunaweza kuzuia karatasi kuingia.

  5. Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi.

  6. Toa trei ya kushikilia nakala zinazochapishwa.

    Kumbuka:

    Rudisha karatasi zinazosalia kwenye paketi. Ukiziwacha katika printa, karatasi hizo zinaweza kukunjika au ubora wa uchapishaji unaweza kupungua.