> Kutatua Matatizo > Karatasi Zinakwama > Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Tahadhari:

Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi. Ikiwa kichapishi kitaanza kufanya kazi, inaweza kusababisha majeraha. Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.

  1. Ondoa karatasi iliyokwama.

  2. Inua paneli dhibiti.

  3. Fungua kifuniko cha ndani.

  4. Fungua kitengo cha kitambazaji hadi kitoe mbofyo.

    Tahadhari:

    Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

    Muhimu:

    Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye mfano ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  5. Ondoa karatasi iliyokwama.

    Muhimu:

    Usiguse sehemu zinazoonyeshwa kwenye mfano ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  6. Funga kitengo cha kitambazaji.

    Kwa usalama, kitengo cha kitambazaji kinafungwa kwa hatua mbili.

    Kumbuka:

    Lazima kitengo cha kitambazaji kiwe kimefungwa kabisa kabla ya kufunguka tena.

  7. Funga kifuniko cha ndani.

  8. Fungua paneli dhibiti.