Unaweza kutafuta menyu kwenye paneli dhibiti ya kichapishi hapa chini:
Mipangilio > Mipangilio ya Faksi > Mipangilio ya Kupokea
Menyu ya Mipangilio ya Kupokea
Hif'hi k. Kompyuta
Huhifadhi faksi zilizopokewa kama faili za PDF kwenye kompyuta iliyounganishwa kwenye kichapishi. Unaweza kuweka hii kwenye Ndiyo kwa kutumia tu FAX Utility (programu tumizi). Huwezi kuwezesha hii kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Sakinisha FAX Utility kwenye kompyuta mapema. Baada ya kuweka hii kwa Ndiyo, unaweza kubadilisha hii kuwa Ndiyo na Uchapishe kutoka kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.
Upunguzaji Otomatiki
Huchapisha faksi zilizopokewa kwa nyaraka za ukubwa zaidi uliopunguzwa ili kutoshea kwenye chanzo cha karatasi. Upunguzaji huenda usiwezekane kulingana na data iliyopokewa. Ikiwa kipengele hiki kimezimwa, hati kubwa huchapishwa kwa ukubwa wake asili kwenye karatasi nyingi, au ukurasa tupu wa pili unaweza kutolewa.
Mip. Kug'ya Ukurasa
Huchapisha faksi zilizopokewa kwa ya kugawa ukurasa wakati ukubwa wa nyaraka ni kubwa kuliko ukubwa wa karatasi iliyopakiwa kwenye kichapishi.
Uzun'ji Otomatiki
Huzungusha faksi zilizopokewa kama mwelekeo wa ulalo nyaraka za ukubwa wa A5 ili iweze kuchapishwa kwenye karatasi ya ukubwa wa A5. Mpangilio huu unatekelezwa wakati mpangilio wa ukubwa wa karatasi kwa angalau chanzo kimoja cha karatasi kinachotumika kwa kuchapisha faksi kimewekwa kwa A5.
Kwa kuteua Zima, faksi zilizopokewa za ukubwa wa mwelekeo wa ulalo wa A5, ambazo zina upana sawa kama nyaraka za ulalo za A4, zinachukuliwa kuwa faksi za ukubwa wa A4 na kuchapishwa vivyo hivyo.
Angalia mpangilio wa ukubwa wa karatasi kwenye Mipangilio > Usanidi wa Printa > Mip'o Chanzo Karatasi.
Ongeza Maelezo ya Mapokezi
Maelezo ya mapokezi ya uchapisho kwenye faksi iliyopokewa, hata iwapo mtumaji hajaweka maelezo ya kichwa. Maelezo ya mapokezi yanajumuisha tarehe na saa, Kitambulisho cha mtumaji, na nambari ya ukurasa (kama vile “P1”). Wakati Mip. Kug'ya Ukurasa imewezeshwa, nambari ya kugawanya ukurasa pia inajumuishwa.
Muda Kuanza Ku'ha
Teua chaguao ili kuanza kuchapisha faksi za kupokea.
Kurasa Zote Zilizopokewa: Uchapishaji huanza baada ya kupokea kurasa zote. Ili kuanza kuchapisha kutoka kwenye ukurasa wa kwanza au ukurasa wa mwisho hutegemea na mpangilio wa kipengele cha Kitita cha Ulinganisho. Tazama ufafanuzi wa Kitita cha Ulinganisho.
Ukurasa wa Kwanza Umepokewa: Huanza kuchapisha ukurasa wa kwanza kupokewa, na kisha huchapisha kwa utaratibu kama kurasa zinapokewa. Iwapo kichapishi hakiwezi kuchapisha, kama vile wakati inachapisha kazi nyingine, kichapishi huanza kuchapisha kurasa zilizopokewa kama bechi zinapopatikana.
Kitita cha Ulinganisho
Kwa kuwa ukurasa wa kwanza unachapishwa mwisho (towe upande wa juu), nyaraka zilizochapishwa zinawekwa pamoja kwenye utaratibu sahihi wa ukurasa. Wakati kumbukumbu ya printa inapungua, kipegele hiki huenda kizipatikane.
Muda Kuk'a K'isha
Wakati wa kipindi fulani cha muda uliobainisha kutoka Muda Kuk. kupitia Washa tena uliyobainisha, kichapishi huhifadhi nyaraka zilizopokewa kwenye kumbukumbu ya kichapishi bila kuzichapisha. Kipengele hiki kinaweza kutumiwa kuzuia kelele usiku au kuzuia hati za usiri kufichuliwa wakati uko mbali. Kabla ya kutumia kipengele hiki, hakikisha kuna kumbukumbu ya kutosha. Unapoweka hii kwa Zima, unaweza kuchapisha nyaraka zilizopokewa hata kabla ya muda wa kuwasha.
Hali Tulivu
Hupunguza kelele ambazo kichapishi hutoa unapochapisha faksi, hata hivyo, kasi ya kuchapisha inaweza kupunguzwa.