> Kunakili > Mbinu Zinazopatikana za Kunakili > Kunakili kadi ya Kitambulisho

Kunakili kadi ya Kitambulisho

Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi yenye ukubwa wa A4.

  1. Teua Nakili kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Weka idadi ya nakala.

  3. Teua nakala ya rangi au nakala ya rangi moja.

  4. Bonyeza kitufe cha OK, na kisha ubonyese kitufe cha .

  5. Teua Nakala ya Kadi ya ID ukitumia vitufe vya , na kisha uteue Washa.

  6. Bonyeza kitufe cha OK, na kisha ubonyese kitufe cha .

  7. Weka nakala ya kwanza ikiangalia chini na uitelezeshe hadi kwa alama ya kona.

    Weka kadi ya Kitambulisho kwa umbali wa 5 mm kutoka kwenye alama ya kona ya glasi ya kitambazaji.

  8. Weka upande wa nyuma wa sura asili chini, itelezeshe kwenye alama ya kona, na kisha ubonyeze kitufe cha .