Kuendesha Usafishaji wa Nishati

Huduma ya Usafishaji wa Nishati hukuwezesha kubadilisha wino wote ulio ndani ya tubu za wino. Katika hali zifuatazo, unaweza kuihitaji kutumia kipengele hiki ili kuboresha ubora wa chapisho.

  • Ulichapisha au kutekeleza usafishaji wa kichwa wakati viwango vya wino vilikuwa chini ili kuonekana kwenye madirisha ya tanki za wino.

  • Ulipofanya ukaguaji nozeli na usafishaji wa kichwa mara 3 na kisha ukasubiri angalau saa 12 bila kuchapisha, lakini bado ubora wa chapisho haukuimarika.

Kabla ya kuendesha kipengele hiki, soma maagizo yafuatayo.

Muhimu:

Hakikisha kuwa kuna wino wa kutosha kwenye tanki za wino.

Hakikisha kuwa tanki zote zina angalau theluthi moja ya wino.Viwango vya chini vya wino wakati wa Usafishaji wa Nishati vinaweza kuharibu bidhaa.

Muhimu:

Kipindi cha saa 12 kinahitajika kati ya kila Usafishaji wa Nishati.

Kwa kawida, Usafishaji wa Nishati moja inafaa kutatua suala la ubora wa kuchapisha ndani ya saa 12.Kwa hivyo, ili kuzuia matumizi yasiyofaa ya wino, unafaa kusubiri hadi saa 12 kabla ujaribu tena.

Muhimu:

Kipengele hiki huathiri maisha ya huduma ya padi za wino.Padi za wino hufikia ukubwa wake mapema kwa kuendesha kipengele hiki.Iwapo padi za wino zimefikia mwisho wake wa maisha, wasiliana na Auni ya Epson ili kuomba mabadiliko.

Kumbuka:

Wakati viwango vya wino havitoshi Usafishaji wa Nishati, huwezi kuendesha kipengele hiki.Hata katika hali hii, viwango vya kuchapisha vinaweza kusalia.

  1. Teua Matengenezo kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Usafishaji wa Nishati.

  3. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuendesha kipengele cha Usafishaji wa Nishati.

    Kumbuka:

    Iwapo huwezi kuendesha kipengele hiki, tatua matatizo yanayoonyeshwa kwenye skrini. Pili, fuata utaratibu kutoka hatua ya 1 ili kuendesha kipengele hiki tena.

  4. Baada ya kuendesha kipengele hiki, endesha ukaguaji nozeli ili kuhakikisha nozeli hazijaziba.

    Kwa maelezo kuhusu jinsi ya kuendesha ukaguzi wa nozeli, tazama maelezo husiani hapa chini.

Muhimu:

Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kuendesha Usafishaji wa Nishati, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha kisha uchapishe ruwaza ya uangaliaji nozeli tena. Endesha Usafishaji Kichwa au Usafishaji wa Nishati tena kwa kutegemea ruwaza iliyochapishwa. Ikiwa ubora bado hajuaimarika, wasiliana na timu ya usaidizi ya Epson.

Kumbuka:

Pia unaweza kuendesha usafishaji wa nishati kutoka kwenye kiendeshi cha kichapishi.

  • Windows

    Bofya Usafishaji wa Nishati kwenye kichupo cha Utunzaji.

  • Mac OS

    Apple menyu > Mapendeleo ya Mfumo > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi) > Epson(XXXX) > Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishaji > Usafishaji wa Nishati