Suluhisho
Ikiwa sauti za operesheni iko juu sana, wezesha Modi Tulivu. Kuwezesha kipengele hiki kunaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.
Kiendeshi cha kichapishi Windows
Wezesha Modi Tulivu kwenye kichupo cha Kuu.
Kiendeshi cha kichapishi Mac OS
Teua Mapendeleo ya Mfumo kwenye menyu ya Apple > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi), na kisha uteue kichapishi. Bofya Chaguo na Usambazaji > Chaguo (au Kiendeshi). Teua On kama mpangilio wa Modi Tulivu.