Wakati karatasi haijaingizwa vizuri, safisha rola ndani.
Bonyeza kitufe cha
ili uzime kichapishi.
Tenganisha waya ya nishati.
Fungua kifuniko cha kichapishi.
Unaweza kupata rola ya kuchukua ndani ya eneo lililoashiriwa kwenye maelezo yafuatayo.
Ondoa rola ya kuchukua.
Bonyeza kichupo kilicho upande wa kulia wa rola ya kuchukua, itelezeshe kuelekea nyuma, na kisha uinue juu wima.
Lowesha kitambaa laini na maji, kikaushe maji vizuri, na kisha upanguze sehemu ya rola yenye nyenzo ya mpira ukiipanguza kwelekea mwelekeo mmoja.
Usiguze sehemu yenye nyezo ya mpira kwenye rola ya kuchukua.
Bonyeza kichupo kilicho upande wa kulia, na kisha upange katika mstari sehemu zilizotokea nje zilizo na mashimo ya kuziambatisha pamoja.
Funga kifuniko cha kichapishi.
Unganisha waya ya nishati.
Bonyeza kitufe cha
ili kuwasha kichapishi.
Ikiwa tatizo halijasuluhishwa, badilisha rola ya kuchukua.