> Katika Hali Hizi > Kusakinisha Programu Kando

Kusakinisha Programu Kando

Unganisha kompyuta yako kwenye mtandao na usakinishe toleo jipya la programu kutoka kwenye tovuti. Ingia kwenye kompyuta yako kama msimamizi. Ingiza nywila ya msimamizi iwapo kompyuta itakuitisha.

Kumbuka:

Wakati unasakinisha upya programu, unahitaji kuisakinusha kwanza.

  1. Hakikisha kuwa kichapishi na kompyuta zinapatikana kwa mawasiliano, na kompyuta imeunganishwa kwenye Intaneti.

  2. Anzisha Epson Software Updater.

    Picha ya skrini ni mfano kwenye Windows.

  3. Kwa Windows, teua kichapishi chako, kisha ubofye ili utafute programu za hivi punde zinazopatikana.

  4. Teua vipengee unavyotaka kusakinisha au kusasisha, na kisha ubofye kitufe cha kusakinisha.

    Muhimu:

    Usizime au kuchomoa kichapishi hadi usasishaji ukamilike. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kichapishi kutofanya kazi.

    Kumbuka:
    • Unaweza kupakua programu-tumizi za sasa kutoka kwenye tovuti ya Epson.

      http://www.epson.com

    • Iwapo unatumia mifumo ya uendeshaji ya Windows Server, huwezi kutumia Epson Software Updater. Pakua programu za hivi majuzi kutoka kwenye tovuti ya Epson.