Wakati uchapishaji una uchafu au kuchakaa, safisha kibiringizaji kiicho ndani.
Unahitaji vipengele vinavyofuata ili kutenda taratibu kutoka kwa hatua ya 2.
kijiti chembamba
shashi au nguo yenye maji iliyokamuliwa vizuri
Tekeleza Usafishaji wa Mwongozo wa Karatasi kutoka kwa kiendeshi cha kichapishi ili kusafisha njia ya karatasi.
Rudia utaratibu ulio hapo juu hadi karatasi iwache kuchafuliwa na wino. Iwapo karatasi itaendelea kupata uchafu kwa wino hata baada ya kusafisha mara kadhaa, nenda kwenye hatua inayofuata.
Kunja shashi au nguo yenye maji iliyokamuliwa vizuri kwenye ncha ya kijiti chembamba.
Zima kichapishi kwa kubonyeza kitufe cha
.
Chomoa waya ya nishati, na kisha ukate muunganisho wa waya ya nishati.
Toa trei ya kushikilia nakala zinazochapishwa.
Tumia kijiti hicho ulichoandaa katika hatua ya 2 kupangusa rola hizo mbili nyeupe kwa kuzizungusha.
Usitumie karatasi ya shashi kusafisha ndani ya kichapishi. Nozeli za kichwa cha kushapisha zinaweza kuzibwa na nyuzi za pamba.
Unganisha waya ya nishati, na kisha uwashe kichapishi.
Ikiwa machapisho bado yamepakwa wino rudia hatua ya 1.