Kutengeneza Bango Kwa Kutumia Alama Zinazolandana za Kupanga

Huu ni mfano wa jinsi ya kutengeneza bango wakati Bango la 2x2 iimechaguliwa, na Alama za Mpangilio Zinazopishana imechaguliwa katika Chapisha Miongozo ya Kukata.

  1. Andaa Sheet 1 na Sheet 2. Kata pambizo za Sheet 1 kwenye mstari wima wa bluu kupitia katikati mwa alama za msalaba za juu na chini.

  2. Weka ukingo wa Sheet 1 juu ya Sheet 2 na upange alama za msalaba, kisha uunganishe karatasi mbili pamoja kwa muda kutoka nyuma ukitumia utepe.

  3. Kata karatasi zilizounganishwa mara mbili katika mstari wima wa bluu kupitia alama za kupanga (wakati huu, mstari upande wa kusho mwa alama za msalaba).

  4. Unganisha karatasi pamoja kutoka nyuma ukitumia utepe.

  5. Rudia hatua 1 hadi 4 uunganishe Sheet 3 na Sheet 4 pamoja ukitumia utepe.

  6. Kata pambizo za Sheet 1 na Sheet 2 katika mstari mlalo wa bluu kupitia katikati mwa alama za msalaba zilizo upande wa kushoto na kulia.

  7. Weka kingo ya Sheet 1 na Sheet 2 juu ya Sheet 3 na Sheet 4 na upange alamaa za msalaba, na kisha uziunganishe pamoja kwa moda kutoka nyuma.

  8. Kata karatasi zilizounganishwa mara mbili katika mstari mlalo mwekundu kupitia alama za kupanga (wakati hii, mtari ulio juu mwa alama za msalaba).

  9. Unganisha karatasi pamoja kutoka nyuma ukitumia utepe.

  10. Kata pambizo zinazobakia katika mwingozo wa nje.