Epson Australia ingependa kukupa kiwango cha juu cha huduma kwa wateja. Zaidi ya miongozo ya bidhaa yako, tunakupa nyenzo zifuatazo za kupata maelezo:
Nenda kwa kurasa za Wavu wa Walimwengu wa Epson Australia. Ni vizuri kuenda na modemu yako hapa kwa uvinjari wa mara kwa mara! Tovuti hutoa eneo la upakuzi wa viendeshi, maenoe ya kuwasiliana na Epson, maelezo ya bidhaa mpya na usaidizi wa kiufundi (barua pepe).
Simu: 1300-361-054
Eneo la Msaada la Epson limetolewa kama akiba ya mwisho ili kuhakikisha wateja wetu wanafikia ushauri. Opareta walio kwenye Eneo la Msaada wanaweza kukusaidia kusakinisha, kusanidi na kutumia bidhaa yako ya Epson. Wafanyakazi wetu wa Eneo la Msaada kabla ya uuzaji wanaweza kukupatia maelezo kuhusu bidhaa mpya za Epson na ushauri kuhusu pale mchuuzi au ajenti wa ukarabati aliye karibu yupo. Aina nyingi za maulizo hujibiwa hapa.
Tunakuhimiza uwe na maelezo yote muhimu tayari unapopiga simu. Maelezo zaidi unayotayarisha, ndivyo tunaweza kukusaidia kwa haraka kutatua tatizo hilo. Maelezo haya yanajumuisha miongozo ya bidhaa yako ya Epson, aina ya kompyuta, programu endeshi, programu-tumizi, na maelezo yoyote unaona inahitajika.
Epson inapendekeza usitupe kisanduku cha kifaa ili uweze kulitumia kwa usafirishaji wa baadaye. Inapendekezwa pia ulinde tangi ya wino na utepe na uweke kifaa kikiwa kimesimama.