> Kutatua Matatizo > Karatasi Zinakwama > Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Tahadhari:

Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi. Ikiwa kichapishi kitaanza kufanya kazi, inaweza kusababisha majeraha. Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.

  1. Ondoa karatasi iliyokwama kwenye mlisho wa nyuma wa karatasi.

  2. Fungua kifuniko cha kichapishi.

  3. Ondoa karatasi iliyokwama.

    Muhimu:

    Usiguze kebo nyeupe bapa, sehemu angavu, au kufuli la usafirishaji ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  4. Funga kifuniko cha kichapishi.