Pia unaweza kutazama taratibu katika M'ozo Video Mt'ni. Fikia tovuti inayofuata.
https://support.epson.net/publist/vlink.php?code=NPD7036
Ikiwa nozeli zimeziba, uchapishaji unakuwa fifu, mistati inaonekana, au rangi zisizotarajiwa zinaonekana. Ikiwa nozeli zimeziba sana, karatasi tupu itachapishwa. Wakati ubora wa chapisho umepungua, kwanza tumia kipengele cha kukagua nozeli na ukague kama nozeli zimeziba. Ikiwa nozeli zimeziba, safisha kichwa cha kuchapisha.
Usifungue kifuniko cha printa au kuzima printa wakati wa usafishaji wa kichwa. Ikiwa usafisha wa kichwa haujakamilika, huenda usiweze kuchapisha.
Kusafisha kichwa hutumia wino mwingi na unapaswa kufanywa ikiwa ni muhimu tu.
Wakati wino ni kidogo, huenda usiweze kusafisha kichwa cha kuchapisha.
Ikiwa ubora wa chapisho umeimarishwa baada ya kukagua nozeli mara kadhaa na kusafisha kichwa mara 3, subiri angalau saa 12 bila kuchapisha, na kisha ufanye ukaguzi wa nozeli tena. Tunapendekeza uzime kichapishi. Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati. Iwapo bado haujaimarika, wasiliana na auni ya Epson.
Ili kuzuia kichwa cha kuchapisha kisikaue, usichomoe printa wakati nishati imewashwa.
Unaweza kuangalia na kusafisha kichwa cha kuchapisha kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi.
Weka karatasi tupu yenye ukubwa wa A4 katika kichapishi.
Bonyeza kitufe cha
ili uzime kichapishi.
Washa kichapishi ukishikilia kitufe cha
chini, na kisha uwachilie vitufe wakati taa ya nishati inamwekamweka.
Ruwaza ya ukaguzi wa nozeli imechapishwa.
Inaweza kuchukua muda ili kuanza kuchapisha ruwaza ya ukaguaji nozeli.
Angalia ruwaza iliyochapishwa ili kuona iwapo nozeli za kichwa cha kuchapisha zimezibika.

chini kwa sekunde 5 hadi taa ya nishati ianze kumwekamweka.
Inaweza kuchukua muda ili kuanza kusafisha kichwa cha kuchapisha.
Wakati taa ya nishati inawacha kumwekamweka, chapisha ruwaza ya ukaguzi wa nozeli tena. Rudia usafishaji na uchapishaji hadi mistari yote ichapishwe kabisa.
Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kukagua nozeli na kusafisha kichwa mara 3, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha, kisha ukague nozeli tena na urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni inahitajika. Tunapendekeza uzime kichapishi. Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati. Iwapo bado haujaimarika, wasiliana na auni ya Epson.