> Kuchapisha > Kuchapisha Picha > Kuchapisha Picha kutoka kwa Vifaa Maizi > Kuchapisha Ukitumia Epson Print Enabler

Kuchapisha Ukitumia Epson Print Enabler

Unaweza kuchapisha hati, barua pepe, picha au kurasa za wavuti pasiwaya moja kwa moja kutoka katika simu au kompyuta yako kibao Android (Android v 4.4 au jipya zaidi). Kwa kudonoa mara chache tu, kifaa chako cha Android kinaweza kugundua kichapishi cha Epson ambacho kimeunganishwa kwenye mtandao sawa pasiwaya.

Tafuta na usakinishe Epson Print Enabler kutoka Google Play.

Nenda katika Mipangilio kwenye kifaa cha Android, teua Kuchapisha kisha wezesha Epson Print Enabler. Kutoka katika programu ya Android kama vile Chrome, donoa aikoni ya menyu na uchapishe kilicho kwenye skrini.

Kumbuka:

Iwapo hutaona kichapishi chako, donoa Vichapishi Vyote na uteue kichapishi chako.