> Kutatua Matatizo > Ubora wa Uchapishaji Uko Chini > Mistari wa Rangi Hutokea kati ya Umbali wa Takriban 2.5 cm

Mistari wa Rangi Hutokea kati ya Umbali wa Takriban 2.5 cm

Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.

Mipangilio ya aina ya karatasi hailingani na karatasi iliyopakiwa.

Suluhisho

Teua mpangilio unaofaa wa aina ya karatasi kwa aina ya karatasi iliyopakiwa katika kichapishi.

Ubora wa chapisho umewekwa kuwa chini.

Suluhisho

Unapochapisha kwenye karatasi tupu, chapisha kwa kutumia mpangilio wa ubora wa juu.

  • Windows

    Teua Juu kutoka Ubora kwenye kichapishi cha kichupo cha Kuu.

  • Mac OS

    Teua Nzuri kama Print Quality kutoka kwenye menyu ya kidirisha cha Mipangilio ya Kuchapisha.

Mkao wa kichwa cha kuchapisha haujaoana.

Suluhisho

Linganisha kichwa cha kuchapisha.

  • Windows

    Bofya Chapisha Mpangilio wa Kichwa kwenye kichupo cha kienfdeshi cha kichapishi cha Utunzaji.

  • Mac OS

    Teua Mapendeleo ya Mfumo kwenye menyu ya Apple > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi), na kisha uteue kichapishi. Bofya Chaguo na Usambazaji > Matumizi > Fungua Matumizi ya Kichapishi, na kisha bofya Print Head Alignment.