> Kutatua Matatizo > Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Kukagua Taa na Hali ya Kichapishi

Taa kwenye peneli ya udhibiti zinaonyesha hali ya kichapishi.

Hali ya Kawaida

: Washa

Taa

Hali

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi).

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa modi ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).

Hali ya Kosa

Wakati hitilafu zinatokea, taa huwaka au kumwekamweka. Maelezo ya hitilafu huonekana kwenye skrini ya kompyuta.

: Washa

: Inamwekamweka

Taa

Hali

Suluhisho

Hitilafu ya muunganisho wa Wi-Fi imetokea.

Bonyeza kitufe cha ili utatue hitilafu na ujaribu tena.

Hakuna karatsi imewekwa au zaidi ya karatasi moja zimeingizwa kwa wakati mmoja.

Ikiwa mwangaza wa kiashiria hiki unawaka wakati unachapisha diski au kadi ya kitambulisho cha PVC, ingiza trei ya diski/kadi ya kitambulisho vizuri.

Baada ya kupakia karatasi au kuingiza trei ya diski/kadi ya kitambulisho vizuri, bonyeza kitufe cha ili kuendelea kuchapisha.

Kukwama kwa karatasi kumetokea au diski au kadi ya kitambulisho cha PVC haijawekwa kwenye trei ya diski/kadi ya kitambulisho vizuri.

Baada ya kuondoa karatasi au kubadilisha kadi ya kitambulisho cha PVC, bonyeza kitufe cha ili kuendelea kuchapisha.

Huenda ujazaji wa wino wa mwanzo haujakamilika.

Angalia bango la Anza Hapa ukamilishe ujazaji wa wino wa mwanzo.

Kikasha cha matengenezo kimekaribia mwisho wa huduma yake.

Mwangaza utaendelea kumweka hadi kikasha cha matengenezo kibadilishwe.

Unaweza kuendelea kuchapisha hadi miangaza ya na imweke moja baada ingine.

  • Kichapishi hakikuzimwa vilivyo.*

  • Kwa kuwa kichapishi kilixzimwa kilipokuwa kikiendesha shughuli, huenda nozeli zimekauka na kuziba.

* Nishati ilizimwa kwa uknada au kitenganishaji cha nishati, plagi iliondolewa kwenye towe, au tatizo la umeme lilitokea.

  • Baada ya kuondoa kosa kwa kubonyeza kitufe cha , tunapendekeza utekeleze ukakuaji nozeli.

  • Ili kuzima kichapishi, hakikisha umebonyeza kitufe cha .

Kumweka moja baada ya nyingine:

Padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Pedi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mipaka inahitaji kubadilishwa.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili kubadlisha pedi ya wino ya uchapishaji usio na mpaka *. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Wakati ujumbe unaosema kwamba unaweza kuendelea kuchapisha unaonekana kwenye kompyuta, bonyeza ili uendelee kuchapisha. Taa zitawacha kumwekamweka kwa muda, hata hivyo, zitaendelea kumwekamweka mara kwa mara hadi padi ya wino ibadilishwe.

Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana.

Kumweka sawia:

Pedi ya wino iko karibu au imefikisha mwisho wa huduma yake.

Pedi ya wino inahitaji kubadilishwa. Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson ili ubadilishe pedi ya wino. Pedi za wino sio vyombo vinavyoweza kukarabatiwa.

Angalia ujumbe ulioonyeshwa kwenye kompyuta, na kisha ubonyeze kitufe cha ili kuondoa hitilafu au ili kuendelea na usafishaji.

Iwapo padi za wino zimefikia mwisho wake wa kutoa huduma, hauwezi tena kutekeleza usafishaji. Uchapishaji unaweza kutekelezwa lakini ubora wa machapisho hauwezi kuahidiwa.

Kufuli la usafirishaji imefungwa.

Baada ya kufungua kufuli la usafirishaji, bonyeza kitufe cha ili kuendelea kuchapisha.

Kumweka moja baada ya nyingine:

Mojawapo ya masuala yafuatayo limefanyika tayari:

  • Usafishaji wa Nishati au kusafisha kichwa cha kichapishi hakuwezi kufanyika kwa sababu hakuna nafasi ya kutosha katika kisanduku cha usimamizi.

  • Kisanduku cha usimamizi hakijasakinishwa sahihi.

  • Kisanduku cha usimamizi kipo mwishoni mwa kipindi chake cha kuhudumu.

Fanya mojawapo ya yafuatayo.

Unapoendesha Usafishaji wa Nishati au kusafisha kichwa cha kichapishi:

  • Badilisha kisanduku cha usimamizi, bonyeza kitufe cha ili kuondoa hitilafu hiyo, na kisha ujaribu tena.

  • Bonyeza kitufe cha ili kuondoa hitilafu hiyo iwapo huwezi kuandaa kisanduku cha usimamizi cha kubadilisha mara moja. Kuchapisha kunaweza kufanyika lakini ubora wa uchapishaji hauwezi kuahidiwa. Hitilafu ikiendelea kufanyika, badilisha kisanduku cha usimamizi, na kisha ubonyeze kitufe cha .

Kando na iliyo hapo juu:

Baada ya kusakinisha tena kisanduku cha usimamizi sahihi, bonyeza kitufe cha .

Hitilafu ikiendelea kufanyika baada ya kusakinisha upya, badilisha kisanduku cha usimamizi, na kisha ubonyeze kitufe cha .

Trei ya towe imetolewa nje.

Toa trei nje.

Miangaza yote itawaka isipokuwa mwangaza wa .

Kichapishi kimeanza katika modi ya kurejesha kwa sababu sasisho la programu msingi halijafaulu.

Fuata hatua zilizo hapa chini ujaribu kusasisha ngome tena.

1. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya USB. (Wakati wa modi ya kurejesha, huwezi kusasisha programu msingi kupitia muunganisho wa mtandao.)

2. Tembelea tovuti yako ya Epson kwa maelekezo zaidi.

Miangaza yote itawaka ikijumuisha mwangaza wa .

Hitilafu ya printa imetokea.

Ondoa karatasi yoyote ndani ya printa. Zima na uwashe printa tena.

Ikiwa hitilafu itaendelea kuonekana baada ya kuzima nishati na kuwasha tena, wasiliana na usaidizi wa Epson.

* Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mpaka. Ili kuzuia uvujaji wa wino kutoka kwenye padi, bidhaa hii imeundwa kusimamisha uchapishaji usiokuwa na mpaka wakati padi imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha ukitumia chaguo la kuchapisha bila kingo. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.