Herufi Zilizochapishwa Sio Sahihi au Zimechanganywa
Sababu zifuatazo zinaweza kuzingatiwa.
Kebo ya USB haijaunganishwa ipasavyo.
Suluhisho
Unganisha kebo ya USB vizuri kwenye kichapishi na kompyuta.
Kuna shughuli inayosuburi kuchapishwa.
Suluhisho
Katisha uchapishaji wowote uliositishwa.
Kompyuta imewekwa kwa modi ya Sinzia au Lala huku ikichapisha.
Suluhisho
Usiweke kompyuta kwenye modi ya Sinzia au modi ya Lala mwenyewe wakati wa kuchapisha. Kurasa za maandishi yaliyochanganywa huenda yakachapishwa wakati ujao unapowasha kompyuta.