> Maelekezo Muhimu > Maagizo ya Usalama > Maagizo ya Usalama ya Wino

Maagizo ya Usalama ya Wino

  • Kwa makini usiguse wino wowote wakatu unashughulikia matangi ya wino, vifuniko vya matangi ya wino, na kufungua chupa za wino au vifuniko vya kwa chupa za wino.

    • Wino ukikumwagikiwa kwenye ngozi, safisha sehemu hiyo vizuri ukitumia sabuni na maji.

    • Wino ukiingia ndani ya macho yako, yamwagie maji mara moja. Maumivu au matatizo ya kuona yakiendelea baada ya kuyamwagia maji, mtembelee daktari mara moja.

    • Wino ukiingia mdomoni mwako, mtembelee daktari mara moja.

  • Usifungue kisanduku cha ukarabati, la sivyo wino unaweza kuingia ndani ya macho yako au kukumwagikia kwenye ngozi.

  • Usitingishe chupa ya wino haraka zaidi au aithirike kwa mipigo ya vifaa kwa kuwa hii inawesza kusababisha uvujaji wa wino.

  • Weka katriji za wino na kisanduku cha matengenezo mbali na watoto. Usiruhusu watoto kunywa kutoka kwa chupa za wino.