> Kutatua Matatizo > Ni Wakati wa Kujaza tena Wino > Tahadhari za Kushughulikia Chupa ya Wino

Tahadhari za Kushughulikia Chupa ya Wino

Soma maelekezo yafuatayo kabla ya kujaza wino upya.

Kuhifadhi tahadhari kwa wino
  • Weka chupa za wino nje ya mwale wa jua wa moja kwa moja.

  • Usihifadhi chupa za wino katika halijoto za juu au zinazoganda.

  • Epson inapendekeza utumie chupa ya wino kabla ya tarehe iliyochapishwa kwenye pakiti.

  • Wakati wa kuhifadhi au kusafirisha chupa ya wino, usiinamishe chupa na usiigongeshe au kuiweka mahali penye mabadiliko ya hali joto.La sivyo, wino unaweza kuvuja hata kama kifuniko kilicho kwenye chupa ya wino kimekazwa vizuri.Hakikisha umeweka chupa ya wino ikiwa imesimama wakati unakaza kifuniko, na utahadhari ili uzuie wino usivuje wakati unasafirisha chupa, kwa mfano, kuweka chupa kwenye mkoba.

  • Baada ya kuleta chupa ya wino ndani kutoka eneo baridi la uhifadhi, iwache ipate joto katika halijoto ya chumba kwa angalau saa tatu kabla ya kuitumia.

  • Usifungue pakiti ya chupa ya wino hadi uwe tayari kujaza tangi la wino.Chupa ya wino hupakiwa bila hewa ili kudumisha utumikaji wake.Ukiwacha chupa ya wino bila kuipakia kwa muda mrefu kabla ya kuitumia, uchapishaji wa kawaida huenda usiwezekane.

  • Pindi unapofungua chupa ya wino, tunapendekeza uitumie haraka iwezekanavyo.

Kushughulikia tahadhari kwa kujaza wino
  • Kwa matokeo bora ya kuchapisha usitumie viwango vya wino vilivyo chini kwa vipindi virefu vya muda.

  • tumia chupa za wino zilizo na msimbo sahihi wa sehemu ya printa hii.

  • Wino wa kichapishi hiki unafaa kushughulikiwa kwa uangalifu. Wino unaweza kumwagika wakati matanki ya wino yamejazwa au kujazwa upya na wino. Ikiwa wino utamwagikia nguo au vitu vyako, huenda usitoke.

  • Usitingishe haraka zaidi au kufinyaza chupa za wino.

  • Ikiwa matangi ya wino hayajaa hadi mstari wa chini, jaza wino upya. Kuendelea kutumia printa kwa muda mrefu wakati kiwango cha wino kiko chini ya laini ya chini kunaweza kuharibu printa.

Matumizi ya wino
  • Ili kudumisha utendaji mzuri wa kichwa cha kuchapisha, kiasi fulani cha wino hutumiwa kutoka kwenye tanki zote wakati wa operesheni za matengenezo kama vile usafishaji wa kichwa cha kuchapisha. Huenda pia wino ukatumika unapowasha kichapishi.

  • Wakati unachapisha rangi moja au kijivujivu, wino wa rangu badala ya wino mweusi unaweza kutumiwa kulingana na aina ya karatasi au mipangilio ya ubora wa uchapishaji. Hii ni kwa sababu mchanganyiko wa wino wa rangu unatumiwa kutengeneza rangi nyeusi.

  • Kiasi fulani cha wino ulio ndani ya chupa za wino ulikuja na printa yako hutumiwa wakati wa usanidi wa mwanzo.Ili uchapishe nakala za hali ya juu, kichwa cha kuchapisha kilicho katika printa yako kitajazwa wino.Mchakato huu wa mara moja hutumia kiasi cha wino na basi chupa hizi zinaweza kuchapisha kurasa chache kulingana na chupa za wino zitakazofuata.

  • Viwango viliandikwa vinaweza kuwa tofauti kulingana na picha unazochapisha, aina ya karatasi unayotumia, marudio ya uchapishaji na hali ya mazingisa kama vile halijoto.