Kubadilisha Muunganisho wa Mtandao kutoka Wi-Fi hadi Ethaneti

Fuata hatua zilizo hapa chini ili kubadilisha muunganisho kutoka Wi-Fi hadi muunganisho wa Ethaneti.

  1. Donoa Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.

  2. Donoa Mipangilio ya Mtandao > Usanidi wa Lana ya Waya.

  3. Donoa Anza Kusanidi.

  4. Angalia ujumbe, kisha udonoe Sawa.

  5. Unganisha kichapishi kwenye kipanga njia kwa kutumia kebo ya Ethaneti.