> Kunakili > Kunakili kadi ya Kitambulisho

Kunakili kadi ya Kitambulisho

Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi yenye ukubwa wa A4.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kuweka Karatasi

  2. Weka nakala ya kwanza ikiangalia chini na uitelezeshe hadi kwa alama ya kona.

    Weka kadi ya Kitambulisho kwa umbali wa 5 mm kutoka kwenye alama ya kona ya glasi ya kitambazaji.

  3. Teua Chapa mbalimbali kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua Nakala mbalimbali > Kadi ya Kitambulisho.

  5. Bainisha asili na ukubwa wa karatasi, na kisha uteue Sawa.

  6. Chagua kichupio cha Nakili.

  7. Donoa .

    Kumbuka:

    Iwapo utadonoa Hakiki, unaweza kuangalia taswira zilizotambazwa.

  8. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kuweka sehemu ya nyuma ya nakala asili, kisha udonoe Anza Kutambaza.

    Weka kadi ya Kitambulisho kwa umbali wa 5 mm kutoka kwenye alama ya kona ya glasi ya kitambazaji.

    Kumbuka:

    Rangi, ukubwa, na ukingo wa taswira iliyonakiliwa ni tofauti kiasi kutoka kwenye nakala asili.