> Kutatua Matatizo > Ujumbe unaonyeshwa kwenye Skrini ya LCD

Ujumbe unaonyeshwa kwenye Skrini ya LCD

Ikiwa ujumbe wa tatizo utaonyeshwa kwenye skrini ya LCD, fuata maelekezo kwenye skrini au suluhu zilizo hapa chini kutatua tatizo.

Ujumbe wa Hitilafu

Suluhisho

Mchanganyiko wa anwani ya IP na Barakoa ya Subnet si sahihi. Angalia nyaraka zako kwa maelezo zaidi.

Ingiza anwani sahihi ya IP au kichanganishi chaguo-msingi. Wasiliana na mtu aliyesanidi mtandao kwa usaidizi.

Urekebishaji wa Kichwa cha Kuchapisha Umekatishwa. Kuna tatizo na kichwa cha kuchapisha. Wasiliana na Auni ya Epson.

Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kurudia kuangalia nozeli na kusafisha kichwa mara 3, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha kisha uangalie nozeli tena na urudie usafishaji wa kichwa ikiwa ni muhimu. Tunapendekeza uzime kichapishi ukitumia kitufe cha . Ikiwa ubora wa uchapishaji bado haujaimarika, endesha Usafishaji wa Nishati.

Ikiwa ubora wa chapisho haujaimarika baada ya kuendesha Usafishaji wa Nishati, subiri kwa angalau saa 12 bila kuchapisha kisha uchapishe ruwaza ya uangaliaji nozeli tena. Endesha Safisha kichwa cha chapa au Usafishaji wa Nishati tena kwa kutegemea ruwaza iliyochapishwa. Ikiwa ubora bado hajuaimarika, wasiliana na timu ya usaidizi ya Epson.

Fikia yafuatayo au angalia nyaraka kwa maelezo. Teua [Imethibitishwa] baada ya kuidhinisha.

Iwapo huwezi kuchanganua msimbo wa QR, unganisha kifaa maizi. Angalia yafuatayo kwa maelezo zaidi.

Kuweka Mipangilio ya Kuunganishwa kwenye Kifaa Maizi

Hitilafu ya mawasiliano. Kagua muunganisho.

Unganisha kompyuta na kichapishi vizuri. Iwapo unaunganisha kupitia mtandao, tazama ukurasa unaofafanua mbinu ya muunganisho wa mtandao kutoka kwenye kompyuta.

Iwapo ujumbe wa kosa unaonyeshwa wakati wa utambazaji, hakikisha kuwa Epson ScanSmart imesakinishwa kwenye kompyuta.

Kuweka Mipangilio ya Kuunganisha Kompyuta

Sasisha cheti shina ili utumie huduma za wingu.

Endesha Web Config, na kisha usasishe cheti cha shina.

Kuendesha Web Config Kwenye Kivinjari Wavuti

Ingiza programu ya Epson Event Manager kwenye kompyuta ili utumie kipengele hiki. Angalia nyaraka zako kwa maelezo zaidi.

Sakinisha Epson ScanSmart kwenye kompyuta.

Kusakinisha Programu Kando

Kagua zifuatazo wakati kompyuta haipatikani. - Muunganisho kati ya printa na kompyuta (USB au mtandao) - Usakinishaji wa programu inayostahili - Kompyuta iliyowashwa - Mipangilio ya programu ya ngome na usalama - Tafuta tena Angalia nyaraka zako kwa maelezo zaidi.

Hakikisha kwamba kompyuta imeunganishwa ipasavyo.

Kuangalia Hali Ya Muunganisho

Kuangalia Hali Ya Muunganisho

Hakikisha kwamba Epson ScanSmart imesakinishwa kwenye kompyuta.

Kusakinisha Programu Kando

Angalia kuwa kiendeshi cha printa imesakinishwa kwenye kompyuta na kuwa mipangilio ya kituo ya printa ni sahihi.

Hakikisha kuwa tundu la kichapishi limeteuliwa vizuri katika Sifa > Tundu kutoka kwenye menyu ya Kichapishi kama ifuatavyo.

Teua “USBXXX” kwa muunganisho wa USB, au “EpsonNet Print Port” ili Kuangalia kwamba kiendesha kichapishi kimesakinishwa kwenye muunganisho wa mtandao.

Angalia kuwa kiendeshi cha printa imesakinishwa kwenye kompyuta na kuwa mipangilio ya kituo cha USB cha printa ni sahihi.

Usanidi wa Karatasi Imezimwa. Baadhi ya vipengele vinaweza kokosekana. Kwa maelezo, angalia nyaraka.

Ikiwa Usanidi wa Karatasi imelemazwa, huwezi kutumia AirPrint.

Haiwezi kutumia Kifaa cha Kumbukumbu kilichoingizwa. Angalia nyaraka zako kwa maelezo.

Tumia kifaa cha kumbukumbu kinachotumika kwenye bidhaa.

Ufafanuzi wa Kifaa cha Kumbukumbu

Uchapishaji umekatishwa kwa sababu huenda karatasi ndefu imetemwa kabla ya uchapishaji kuisha.Weka urefu wa karatasi kuwa fupi kuliko 1300 mm.Angalia nyaraka zako kwa maelezo.

Uchapishaji huchukua muda mrefu kwa sababu ya halijoto za juu, na karatasi ndefu inaweza kuondolewa nusu ya uchapishaji.

  • Weka urefu wa karatasi ili iwe fupi kwa 1.3 m.

  • Chapisha kwa halijoto iliyo chini ya 32 °C.

Uchapishaji umekatishwa kwa sababu huenda karatasi ndefu imetemwa kabla ya uchapishaji kuisha.Weka Ubora kwa Kawaida.Angalia nyaraka zako kwa maelezo.

Uchapishaji huchukua muda mrefu kwa sababu ya data kubwa ya uchapishaji, na karatasi ndefu inaweza kuondolewa nusu ya uchapishaji.

Weka Ubora kwenye Kawaida.

Pedi ya wino ya machapisho yasiyo na mipaka ya printa imefikisha mwisho wa matumizi yake. Sio sehemu inayoweza kubadilishwa. Tafadhali wasiliana na auni ya Epson.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili kubadlisha pedi ya wino ya uchapishaji usio na mpaka*. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Uchapishaji usiokuwa na mpaka haupatikani, lakini kuchapisha mpaka kunapatikana.

Kuwasiliana na Usaidizi wa Epson

Pedi ya wino ya machapisho yasiyo na mipaka ya printa inakaribia mwisho wa matumizi yake. Sio sehemu inayoweza kubadilishwa. Tafadhali wasiliana na auni ya Epson.

Wasiliana na Epson au mtoa huduma aliyeidhinishwa wa Epson ili kubadlisha pedi ya wino ya uchapishaji usio na mpaka*. Sio sehemu ya kukarabatiwa na mtumiaji.

Donoa OK ili kuendelea na uchapishaji.

Kuwasiliana na Usaidizi wa Epson

Hitilafu ya Printa

Zima na uwashe nishati tena. Ikiwa tatizo litaendelea, bonyeza "Endelea".

Fanya yafuatayo.

1. Fungua kitengo cha kitambazo na uondoe karatasi yoyote au nyenzo yoyote ya kuilinda ndani ya kichapishi. Safisha utepe nzito ikiwa imechafuka.

Kuondoa Karatasi Iliyokwama

Kusafisha Filamu Angavu

2. Funga kitengo cha kitambazaji na uzime na uwashe nishati.

Ikiwa ujumbe wa hitilafu bado unaonekana baada ya kuzima nishati na kuwasha tena, wasiliana na usaidizi wa Epson.

Kuwasiliana na Usaidizi wa Epson

Kosa limetokea wakati wa kuhifadhi. Angalia na kama inafaa, badilisha kifaa cha kumbukumbu.

Kifaa cha hifadhi ya nje, kama vile kadi ya kumbukumbu, kinaweza kuharibika. Angalia iwapo kifaa kinapatikana.

Ufafanuzi wa Kifaa cha Kumbukumbu

Haiwezi kugundua midia. Angalia nyaraka zako kwa maelezo zaidi kuhusu midia

Tumia kifaa cha kumbukumbu kinachotumika kwenye bidhaa.

Ufafanuzi wa Kifaa cha Kumbukumbu

Umepakia karatasi ifuatayo kwenye XX?

Badilisha mipangilio ya chapisho au pakia karatasi inayolingana na mipangilio ya chapisho katika kaseti ya karatasi kisha ubadilishe mipangilio ya karatasi.

Iwapo hutaki kuonyesha ujumbe huu kutoka wakati mwingine, teua Mipangilio > Vitendaji vya Mwongozo, na kisha uweke Karatasi Hailingani kwa Zima.

Recovery Mode

Update Firmware

Kichapishi kimeanza katika modi ya kurejesha kwa sababu sasisho la programu msingi halijafaulu. Fuata hatua zilizo hapa chini ujaribu kusasisha ngome tena.

1. Unganisha kompyuta na kichapishi ukitumia kebo ya USB. (Wakati wa modi ya kurejesha, huwezi kusasisha programu msingi kupitia muunganisho wa mtandao.)

2. Tembelea tovuti yako ya Epson kwa maelekezo zaidi.

* Katika baadhi ya mizunguko ya uchapishaji kiasi kidogo sana cha wino wa ziada kinaweza kukusanywa katika padi ya wino ya uchapishaji usiokuwa na mpaka. Ili kuzuia uvujaji wa wino kutoka kwenye padi, bidhaa hii imeundwa kusimamisha uchapishaji usiokuwa na mpaka wakati padi imefikisha kikomo chake. Kuhitajika kwake na mara inayohitajika kutatofautiana kulingana na idadi ya kurasa unazochapisha ukitumia chaguo la kuchapisha bila kingo. Kuhitajika kwa ubadilishaji wa padi hakumaanishi kwamba printa yako imewacha kufanya kazi kulingana na sifa zake. Printa itakuarifu wakati padi inahitajika kubadilishwa na jambo linaweza tu kufanywa na Mtoa huduma aliyeidhinishwa na Epson. Udhamini wa Epson hausimamii gharama ya ubadilishaji huu.