> Kunakili > Kunakili Picha

Kunakili Picha

Unaweza kunakili picha kwa urahisi. Unaweza pia kurejesha rangi ya picha zilizofifia.

Ukubwa wa chini zaidi wa nakala asili unaweza kunakini ni 30×40 mm.

Kumbuka:

Huenda nafasi nyeupe iliyo karibu na picha isitambuliwe.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kuweka Karatasi

  2. Teua Chapa mbalimbali kwenye paneli dhibiti.

  3. Teua Nakala mbalimbali > Nakili/Rejesha Picha.

  4. Badilisha mipangilio ya kuchapisha inavyohitajika, na kisha uteue Kuweka Nakala Asili.

    Chaguo za Menyu ya Karatasi na Mipangilio ya Kuchapisha kwa Picha za Kunakili

  5. Weka nakala ya kwanza ikiangalia chini na uitelezeshe hadi kwa alama ya kona.

    Weka picha kwa umbali wa 5 mm kutoka kwenye alama ya kona ya glasi ya kichapishi. Unaweza kuweka picha nyingi na picha za ukubwa tofauti.

    Unapoweka picha nyingi, acha nafasi ya angalau 5 mm kati ya picha.

    Ukubwa wa juu: 10×15 cm (4×6 in.)

  6. Teua Anza Kutambaza.

    Picha zinatambazwa na kuonyeshwa kwenye skrini.

  7. Teua Hariri iwapo inahitajika kuunda mipangilio kama vile marekebisho ya picha.

    Kumbuka:

    Iwapo unataka kuchapisha kwa kuongeza ukubwa wa sehemu ya picha, teua Puna/Kuza, na kisha uunde mipangilio. Telezesha fremu ya ebeo la kuchapisha upande wa kushoto, na kisha ubadilishe ukubwa wa fremu kutumia kwenye kona za fremu.

    Chaguo za Menyu ya Marekebisho ya Picha kwa Kunakili Picha

  8. Donoa .

    Kumbuka:

    Rangi, ukubwa, na ukingo wa taswira iliyonakiliwa ni tofauti kiasi kutoka kwenye nakala asili.