Unaweza kusanidi mtandao wa Wi-Fi kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya. Ikiwa masharti yafuatayo yatatimizwa, unaweza kusanidi kwa kutumia mbinu hii.
Kipanga njia pasiwaya kinatangamana na WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa).
Muunganisho wa sasa wa Wi-Fi ulitambuliwa kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya.
Donoa
kwenye skrini ya nyumbani.
Donoa Wi-Fi (Inapendekezwa).
Iwapo kichapishi tayari kimeunganishwa kwa Ethaneti, donoa Kipangishi njia.
Donoa Anza Kusanidi.
Iwapo tayari muunganisho wa mtandao umesanidiwa, maelezo ya muunganisho yanaonyeshwa. Donoa Badilisha Mipangilio ili kubadilisha mipangilio.
Ikiwa tayari kichapishi kimeunganishwa kupitia Ethaneti, donoa Badilisha kwa muunganisho wa Wi-Fi., kisha udonoe Ndiyo baada ya kuthibitisha ujumbe.
Donoa Sukuma Kitufe cha Usanidi (WPS).
Shikilia chini kitufe cha [WPS] kwenye kipanga njia pasiwaya hadi taa ya usalama imweke.

Ikiwa hujui kilipo kitufe cha [WPS], au hakuna vitufe kwenye kipanga njia pasiwaya, tazama hati iliyotolewa yenye kipamnga njia pasiwaya kwa maelezo.
Donoa Anza Kusanidi.
Donoa Funga.
Skrini hufunga kiotomatiki baada ya kipindi maalum cha muda iwapo hutadonoa Funga.
Iwapo muunganisho utashindikana, washa upya kipanmga njia pasiwaya, kisogeze karibu na kichapishi, na ujaribu tena. Iwapo haitafanya kazi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na uangalie suluhisho.
Donoa Funga kwenye skrini ya mipangilio ya muunganisho wa mtandao.