Unaweza kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili kuangalia hali kati ya kichapishi na kipanga njia pasiwaya.
Pakia karatasi.
Donoa Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.
Donoa Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho.
Ukaguzi wa muunganisho unaanza.
Donoa Chapisha Ripoti ya Ukaguzi.
Fuata maagizo kwenye skrini ya kichapishi ili kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.
Iwapo kosa limetokea, angalia ripoti ya muunganisho, na kisha ufuate suluhisho zilizochapishwa.
Donoa Funga.