> Kuchapisha > Kuchapisha Vipengee Mbalimbali > Kuchapisha Karatasi ya Kuandika

Kuchapisha Karatasi ya Kuandika

Unaweza kuchapisha karatasi asili ya kuandika kwa urahisi kkwa picha kutoka kwa kifaa cha kumbukumbu kilichowekwa kama mandharinyuma. Picha hii imechapishwa kihafifu ili kuwa inaweza kuandikwa juu kwa urahisi.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kuweka Karatasi

  2. Chomeka kifaa cha kumbukumbu kwenye sloti ya kadi ya SD au kiweko cha USB cha kiolesura cha nje cha kichapishi.

    Kuchomeka na Kuondoa Kadi ya Kumbukumbu

    Kuchomeka na Kuondoa Kifaa cha Nje cha USB

  3. Teua Chapa mbalimbali kwenye paneli dhibiti.

  4. Teua Vifaa vya kuandikia > Karatasi za Kuandikia.

  5. Teua aina ya karatasi ya kuandika.

  6. Teua mandharinyuma.

    Chaguo zinatofautiana kwa kutegelea aina ya karatasi ya kuandika.

  7. Fanya moja kati ya yafuatayo kulinagana mandharinyuma uliyochagua katika hatua ya 6.

    Chaguo zinatofautiana kulinagana na aina ya mandharinyuma.

    • Muundo
      Teua ruwaza, kama vile mipaka au nukta polka au Muundo Asili kisha uteue ruwaza uliyounda kwa kutumia kipengele cha ruwaza ya karatasi.
    • Picha
      Wakati ujumbe unaokuambia kuwa kupakia picha kumekamilika unaonyeshwa, teua Sawa. Teua , teua picha unayotaka kuchapisha kwenye skrini ya kuteua picha kisha uteue Imefanyika. Teua Ifuatayo.
    • Rangi
      Teua rangi ya mandharinyuma.
    • Hakuna Usuli
      Nenda kwa hatua inayofuata.
  8. Unda mipangilio ya karatasi.

  9. Ingiza idadi ya nakala, na kisha udonoe .