> Kuchapisha > Kuchapisha Vipengee Mbalimbali > Kuchapisha Karatasi na Ruwaza (Karatasi Undwa)

Kuchapisha Karatasi na Ruwaza (Karatasi Undwa)

Unaweza kuchapisha aina mbalimbali za karatasi ya ubunifu kwa kutumia ruwaza zilizohifadhiwa kwenye kichapishi, kama vile mipaka na vitone vya polka. Unaweza pia kuchapisha ruwaza asilia na picha kutoka kifaa cha kumbukumbu. Hii hukuruhusu kutumia karatasi katika njia mbalimbali, kama vile kuunda majalada ya vitabu yaliyoundiwa nyumbani, karatasi za kufunga, nakadhalika. Tembelea tovuti ifuatayo kwa maelezo kuhusu jinsi ambavyo unaweza kuunda vipengee vyako mwenyewe.

http://epson.sn

Kumbuka:

Epson Creative Print hukuruhusu kuchapisha karatasi undwa kwa ruwaza mbalimbali.

Programu ya Kufurahia Uchapishaji wa Picha Anuwai (Epson Creative Print)

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kuweka Karatasi

  2. Teua Chapa mbalimbali kwenye paneli dhibiti.

  3. Teua Vifaa vya kuandikia > Karatasi ya uchoraji.

  4. Fanya moja kati ya zifuatazo.

    • Ili kutumia ruwaza zilizohifadhiwa kwenye kichapishi, chagua ruwaza kama vila mipaka na vitone vya polka.
    • Ili kutumia picha zilizohifadhiwa kwenye kifaa cha kumbukumbu, teua, Muundo Asili na kisha uweke kifaa cha kumbukumbu. Ili kuunda ruwaza mpya, chagua Unda, kisha ufuate maelekezo kwenye skrini ili kuchagua na kuhifadhi picha.

    Kuchomeka na Kuondoa Kadi ya Kumbukumbu

    Kuchomeka na Kuondoa Kifaa cha Nje cha USB

  5. Unda mipangilio ya karatasi.

  6. Ingiza idadi ya nakala, na kisha udonoe .