Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini.
Mipangilio > Usanidi wa Printa
Usanidi wa Printa
Mip'o Chanzo Karatasi
Mipangilio ya Karatasi
Chagua ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi uliyoingiza katika chanzo cha karatasi.
A4/Letter Ubad. Ot.
Teua Washa Ili kuweka karatasi kutoka kwa chanzo cha karatasi kilichowekwa ukubwa wa A4 wakati hakuna chanzo cha karatasi kilichowekwa kama Letter, au huweka kutoka kwa chanzo cha karatasi kilichowekwa ukubwa wa Letter ambapo hakuna chanzo cha karatasi kilichowekwa A4.
Ilani ya Hitilafu
Ilani ya Uk'a wa Ka'si
Teua Washa ili kuonyesha ujumbe wa kosa wakati ukubwa wa karatasi ulioteuliwa haufanani na karatasi iliyopakiwa.
IIlani ya Aina ya Karatasi
Teua Washa ili kuonyesha ujumbe wa kosa wakati aina ya karatasi iliyoteuliwa haifanani na karatasi iliyopakiwa.
Ony. Ot. Usan'i/ Kar.
Teua Washa ili kuonyesha skrini ya Mipangilio ya Karatasi unapopakia chanzo cha karatasi. Ukilemaza kipengele hiki, huwezi kuchapisha kutoka kwenye iPhone, iPad au iPod touch ukitumia AirPrint.
Hali Tulivu
Teua Washa ili kupunguza kelele wakati wa kuchapisha, hata hivyo, hii inaweza kupunguza kasi ya uchapishaji. Kulingana na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa kuchapisha uliyoteua, huenda kusiwe na tofauti katika kiwango cha kelele ya kichapishi. Chagua Washa ili kuipa kipaumbele upunguzaji kelele ya shughuli. Ili kuipa kipaumbele kasi ya kuchapisha, chagua Washa (Kiwango cha chini).
Washa Nishati Otomatiki
Teua Washa Nishati Otomatiki ili kuwasha kichapishi kiotomatiki kinapopokea kazi ya kuchapisha au kutambaza kupitia kwa muunganisho wa USB au muunganisho wa mtandao. Hakikisha utoe trei ya towe ili kuzua machapisho yasianguke.
Kuwezesha Washa Nishati Otomatiki huongeza matumizi ya nishati kiasi kwenye hali tuli ikilinganishwa na kuzima kichapishi kikamilifu. Pia inachukua muda mrefu zaidi kuzima nishati. Acha waya ya nishati ichomekwe ndani wakati unatumia kipengele hiki. Ikiwa utachomoa waya ya nishati, hakikisha mwangaza wa nishati umezimwa.
Tumia mpangilio wa Kipima Saa ya Kuzima iwapo unataka kichapishi kuzima kiotomatiki wakati kazi ya kuchapisha au kutambaza imekamilika na kipindi cha muda kilichowekwa kimepita bila operesheni kutekelezwa. Hii ni muhimu wakati uchapishaji kutoka kwa eneo la mali kama vile kupitia mtandao.
Mip'ilio ya Kuzima
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Kipima Saa ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Zima Ikiwa Haitumiki
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki iwapo hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Ongezeko lolote litaathiri ufanisi wa nishati ya bidhaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Zima ikiwa Imetenganishwa
Teua mpangilio huu ili kuzima printa baada ya muda maalum wakati vituo tarishi zote ikijumuisha kituo cha USB kimetenganishwa. Kipengele hiki huenda kisipatiokane kulingana na eneo lako.
Huenda bidhaa yako ina kipengele hiki au kipengele cha Mip'ilio ya Kuzima kulingana na eneo la ununuzi.
Teua mpangilio huu ili kuzima kichapishi kiotomatiki wakati hakijatumiwa kwa kipindi cha muda uliobainishwa. Unaweza kurekebisha muda kabla ya udhibiti wa nishati kutekelezwa. Uongezaji wowote utaathiri utumiaji wa nishati wa kifaa. Tafadhali zingatia mazingira kabla ya kufanya mabadiliko yoyote.
Lugha/Language
Teua lugha inayotumiwa kwenye skrini ya LCD.
Kibodi
Badillisha muundo wa kibodi kwenye skrini ya LCD.
Kipima saa cha Kulala
Rekebisha kipindi cha muda cha kuingia kwenye modi ya kusinzia (modi ya kuhifadhi nishati) wakati kichapishi hakijatekeleza operesheni zozote. Skrini ya LCD inakuwa nyeusi wakati muda uliowekwa unapita.
Muunganisho wa Kompyuta kupitia USB
Teua Wezesha ili kuruhusu kompyuta kufikia kichapishi inapounganishwa kwenye USB. Wakati Lemaza imeteuliwa, uchapishaji na utambazaji ambao haujatumwa kupitia muunganisho wa mtandao unazuiwa.