Badilisha mipangilio ya tambazo ili kupunguza ukubwa wa faili ya taswira iliyotambazwa.
Kiwango kinachoweza kupunguzwa hutofautiana kulingana na nakala asili.
Badilisha umbizo la faili:
Teua umbizo la PDF ili kutambaza nyaraka, na kuteua umbizo la JPEG ili kutambaza picha.
Punguza mwonekano:
Utambazaji wa 200 dpi hutoa ubora wa kutosha unapotambaza nyaraka.