Kuchapisha Taswira fifi

Unaweza kuchapisha taswira fifi kama vile “Ya siri” au ruwaza ya kutonakili kwenye machapisho yako. Iwapo utachapisha kwa ruwaza ya kutonakili, herufi zilizofichwa huonekana zinaponakiliwa ili kutofautisha nakala asili kutoka kwenye nakala.

Ruwaza ya Kizuia Nakala inapatikana chini ya masharti yafuatayo:

  • Karatasai: Karatasi tupu, Karatasi ya nakala, Kichwa cha barua, au Karatasi tupu ya ubora wa juu

  • Ubora: Wastani

  • Urekebishaji wa mlio: Otomatiki

Kumbuka:

Unaweza pia kuongeza taswira fifi yako mwenyewe ya ruwaza ya kutonakili.

  1. Pakia karatasi katika kichapishi.

    Kupakia Karatasi katika Mkanda wa Karatasi

  2. Fungua faili unayotaka kuchapisha.

  3. Nenda kwa dirisha la kiendeshi cha kichapishi.

  4. Bofya Vipengele vya Taswira fifi kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi na uteue ainaya ruwaza ya aina isiyo ya nakala au taswira fifi unayotaka kutumia.

  5. Bofya Mipangilio ili kubadilisha maelezo kama vile ukubwa, uzito, au nafasi ya ruwaza au alama.

  6. Weka vipengele hivyo vingine kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi inavyohitajika, na kisha ubofye SAWA.

    Kichupo cha Kuu

    Kichupo cha Chaguo Zaidi

  7. Bofya Chapisha.